• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mh. Makamu wa Rais amesema " bilioni 42 zimetolewa kwa ajili ya Elimu bure bila malipo.

Tarehe ya kuwekwa: September 16th, 2020

Kauli hiyo imetamkwa hapo jana 15.09.2020 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan  katika Mkutano wa uzinduzi wa Kampeni ya uchaguzi mkuu  unaotarajia kufanyika tarehe 28 octoba mwaka huu uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe Manispaa ya Songea.

Mh. Samia alianza kwa kutoa shukrani kwa wananchi wa Manispaa ya Songea kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi wenye  lengo kuu la kuwaeleza wananchi mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano chini ya uongozi wa Dr. John Pombe Magufuli.

Alisema katika sekta ya kilimo Serikali imejipanga kuagiza pembejeo za kilimo ili wakulima wapate pembejeo kwa wakati  na kwa sifa zinazotakiwa na kwa bei nafuu.

Alisema kwa miaka mitano iliyopita waliweza kushusha bei ya mbolea kutoka shilingi 64,000/= hadi shilingi 46,000/=. Pia Serikali imejipanga kuwezesha uwekezaji wa kilimo cha biashara kwa kuongeza uwezo wa kuhifadhi mazao  gharani na kujenga na kukarabati  maghala yenye tani 531850 pamoja na kuweka mfumo mzuri wa soko la ndani na soko la nje.

Aidha katika sekta ya elimu Mkoa wa Ruvuma umepokea zaidi ya bilioni 26 kwa ajili ya ujenzi, ukamilishaji, na ukarabati kwa Shule za Msingi na Sekondari.

Alisema jumla ya shilingi bili 42 zilitolewa kwa ajili ya elimu bure bila maliopo. Aliongeza kuwa Serikali isingetoa fedha hizi, fedha hizo zingetolewa na wazazi wa wanafunzi, hivyo Serikali ikaona ni vyema sasa fedha hizo zitolewe na Serikali ili kuwapunguzia mzigo huo wazazi kwa ajili ya elimu ya watoto wetu kwa elimu msingi na sekondari.

 Hata hivyo, alifafanua kuwa  Mkoa wa Ruvuma mwaka 2015  ulikuwa na shule za Msingi  670 hadi  kufikia  2020 shule zimeongezeka na kufikia shule 800, pia kwa upande wa shule za sekondari  mwaka 2015  kulikuwa na  shule  111 hadi kufikia mwaka 2020 shule zimeongezeka na kufikia idadi ya  shule 205.

Aliongeza kuwa zaidi ya billion 9 zimetumika kujenga madarasa 433, nyumba za walimu 46, matundu ya vyoo 2369, katika shule za msingi pia kwa upande wa Sekondari Zaidi ya billion 18 zimetumika kujenga madarasa 327, nyumba za walimu 37, matundu ya vyoo 474, mabweni 27, Hosteli 13, Maabara 128, maktaba 4, bwalo za chakula 8, majengo ya utawala 2, na ukarabati wa shule kongwe 4 katika shule za Sekondari.

Aidha baada ya hotuba yake  aliomba kura kwa wananchi kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi ( Rais, Mbunge, na Madiwani) ili waweze kuleta maendeleo ndani ya jimbo la Songea.

Mwisho alichukua ilani ya utekelezaji ya CCM na kumkabidhi mgombea Ubunge wa Jimbo la Songea mjini Dr. Damas Ndumbaro ili aweze kuisimamia na kutekeleza kwa ajili ya wananchi wa Tanzania.

IMEANDALIWA NA;

AMINA PILLY, AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.

16.09.2020.

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Bil. 22.9 Kujenga Masoko ya Kisasa Manzese A na B, na Kiwanda cha Kuchakata Mazao ya Nafaka Lilambo

    July 06, 2025
  • MBUNGE SONGEA MJINI AKABIDHI KOMPYUTA NA KUFADHILI UKARABATI WA OFISI ZA POLISI

    June 27, 2025
  • DC Songea bAzindua Dawati la Huduma za Ustawi wa Jamii Stendi ya Mabasi Songea

    June 24, 2025
  • Meya Mbano; Amewataka Wananchi Kulinda Haki za Watoto

    June 16, 2025
  • Tazama zote

Video

Makabidhiano ya Mkataba Soko la Manzese A&B
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa