MKUU wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema amefanya utalii wa ndani katika nyotamkia au kimondo kilichoanguka mwaka 1840 katika Kijiji cha Ndolezi wilayani Mbozi mkoani Songwe.Serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli imefungua milango ya utalii katika ukanda wa kusini ili kuona serikali na wananchi katika mikoa hiyo inanufaika na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika maeneo hayo.
Hiki ni moja ya vivutio adimu vya utalii nchini ambacho kinawashangaza wengi. Kimondo hiki kilianguka mwaka 1840 katika kijiji cha Ndolezi Wilaya ya Mbozi.Km 62 kutoka Mbeya mjini kabla ya mji wa Mlowo na Vwawa kuna kijiji kinaitwa Mahenje. Kijiji hiki ndio njia panda ya kuelekea kwenye kimondo kijiji cha NDOLEZI kata ya MLANGALI km 12 kutoka barabara kuu ya lami.
Kimondo hiki kinakadiliwa kuwa ndo kimondo kikongwe zaidi kati ya vile vilivyopo sasa duniani. Kina mchanganyiko wa madini mbali mbali kama vile Chuma 90%, Nickel 8%, Copa,salfa na Phosforasi 2%.Hiki kimondo ni cha nne kwa uzito kikiwa na tani 12, cha kwanza chenye uzito wa tani 60 kiko nchini NAMIBIA. Nchi zingine zenye vimondo ni Marekani, Green Land Magharibi, Mexico na Argentina.
Kimondo hiki kwa mara ya kwanza kilivumbuliwa na mwenyeji wa maeneo hayo aliyekuwa muhunzi, alidhani ni jiwe la Chuma lakini alipojaribu kulikata alipata ugumu ambao ulimshangaza zaidi. Muhunzu huyu ambaye alitoa taarifa kwa Chifu wao.Baada ya Chifu kushuhudia lile jiwe la ajabu aliwambia watu wake kuwa ile ilikuwa ni Baraka za Mungu kwa jamii yake hivyo walianza kutambika kukizunguka kile kimondo.
Ilipofika mwaka 1930 alikuja Mjerumani mmoja kutokea Afrika Kusini aliyeitwa William H. Chnot na akaomba wazawa wampeleke kwenye jiwe la maajabu na aligundua lile halikuwa jiwe kama wazawa walivyokuwa wakidhani. Aliomba serikali ya kikolini ya Ujerumani itume wataalamu wake wa miamba ili kufanya utafiti. Walikata kipande kidogo na wakakipeleka Uingereza kwenye maabara. Majibu yalirudi mwaka 1931 na kubaini kwamba kile ni kimondo.
Kimondo hiki ni cha baridi wakati wote kutokana na mchanganyiko wa madini yake. Madini ya chuma kwa kawaida hupokea joto lakini madini ya Nickel hutawanya joto ndo maana ni cha baridi muda wote. Ingawa nickel ni asilimia 8 tu na chuma ni asilimia 90 lakini nickel yana nguvu kuliko chuma kwa kutawanya joto.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa