KAMATI ya lishe ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma, imefanyika kikao leo kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Songea, pamoja na mambo mengine wamezungumzia athari za kiafya zinazotokana na kuhifadhi mahindi na nafaka nyingine kwa kutumia kemikali za maji ambazo zina sumu zinazosababisha magonjwa ya ini na figo.
MTAZAME Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akizungumzia sababu zinazoifanya wilaya ya Nyasa kuwa kitovu cha Utalii katika mkoa wa Ruvuma
MKOA wa Ruvuma sasa utakuwa na migodi miwili, ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe ukiwemo mgodi wa Ngaka wilayani Mbinga na sasa KAMBAS Muhukuru Songea.MGODI upo umbali za zaidi ya kilometa 150 toka mjini Songea.Lengo la Mgodi ni kuzalisha kati ya tani 600 hadi 700 kwa siku ambapo kwa mwezi Mgodi utakuwa na uwezo wa kuzalisha makaa ya mawe kati ya tani 18,000 hadi 21,000 kwa mwezi.Hadi sasa Mgodi wa KAMBAS umetoa ajira rasmi 20 na ajira ambazo sio rasmi 50
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa