Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameongoza mazishi ya baadhi ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere iliyozama Septemba 20, 2018,ambapo hadi kufikia Septemba 23 mwaka huu,watu 123 wamepoteza maisha katika ajali hiyo.
MPAKA kufikia Juni, 2018, upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imefikia asilimia 50.1 sawa na idadi ya watu 45,929 kwa wakazi waishio pembezoni mwa Mji wa Manispaa ya Songea yaani sehemu ambazo Mamlaka ya Maji safi na Taka (SOUWASA) hawajaweza kutoa huduma ya Maji safi na Salama.
Mkuu wa Idara ya Maji katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mhandisi Samwel Sanya anasema Halmashauri mwaka 2007 wakati inaanza kutekeleza programu ya maji ilikuwa na asilimia 17 tu na kwamba tangu mwaka 2007 inaendelea Kutekeleza Programu ya maji na Usafi wa Mazingira katika Mitaa 10 ,awamu ya kwanza ambayo ni Mahilo, Chandarua, Muhombezi, Muungano, Mahinya, Ngandula, Ruhuwiko Kanisani, Mitendewawa, Ruhila kati na Liwumbu.
TAZAMA yaliyojiri katika Mkutano wa Baraza Maalum la madiwani kuwasilisha Taarifa ya Hesabu za kufunga mwaka 2017/2018,kikao ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaj Abdul Hassan Mshaweji
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa