NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashista Ndetiye ametoa maelezo ya mabasi kuanza safari saa 11 alfajiri badala ya saa 12.Mtazame anafafanua zaidi
MTAZAME Mkurugenzi wa Kampuni ya TOPONE ya Songea Pascal Msigwa akielezea sababu za kuanzisha chuo cha ufamasia katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
Mratibu wa Mafunzo ya Chuo hicho David Anderson amesema chuo hicho kinafaa vyote muhimu ambavyo vitatumika kwa wanachuo ikiwemo maabara yenye vifaa vya kutosheleza,maktaba,vyumba vya madarasa na mabweni.Hata hivyo amesema kwa kuanzia chuo hicho kinatarajia kuchukua wanachuo wasiozidi 200 na amezitaja sifa za kujiunga na chuo hicho ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne waliofaulu katika kiwango cha chini ni ufaulu wa D nne kati ya hizo D mbili katika masomo ya Sayansi Biolojia na Kemia na D nyingine mbili katika masomo mengine isipokuwa masomo ya Dini na Biashara.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa