• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

Posted on: April 19th, 2023

Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuomba nafasi za kazi mbalimbali zilizotajwa hapa chini, baada ya kupokea kibali cha Ajira Mpya kwa mwaka 2022/2023 chenye Kumb.Na.FA.97/228/01 “TEMP”/06 cha tarehe 06 Aprili, 2023 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

  • MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 02
  • SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI).
  • Awe na Stashahada (NTA Level 6) katika fani ya urasimu ramani (Cartography) au (geoinformatics),  Sheria, Afya na Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
  • KAZI ZA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – MASJALA ZA KAWAIDA
  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye regista (incoming correspondence register).
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence register).
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers).
  • Kupokea majalada kwa watendaji (action officers).
  • Kupokea majalada yanayorudi masijala toka kwa watendaji.
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (racks/filing cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking).
  •  
  • NGAZI YA MSHAHARA
  • Ngazi ya mshahara ni TGS C.
  • MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 02
  • SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe amehitimu Kidato cha Nne na mwenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya uhazili.  Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile; Word, Excel, Power Point, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
  • KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II
  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri.
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
  • Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine.
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali, na
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
  • NGAZI YA MSHAHARA
  • Ngazi ya mshahara ni TGS C.
  • DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 05
  • SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe amehitimu na mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
  • Awe na Leseni ya Daraja E au C1 ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
  • Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.  Waombaji wenye cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.
  • KAZI ZA DEREVA DARAJA LA II
  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
  • Kufanya usafi wa gari, na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
  • NGAZI YA MSHAHARA
  • Ngazi ya Mshahara ni TGS B.
  • MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III – NAFASI 05
  • SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI).
  • Aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo – Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
  • KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA MTAA
  • Katibu wa Kamati ya Mtaa.
  • Mtendaji Mkuu wa Mtaa.
  • Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa.
  • Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa.
  • Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria Ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa.
  • Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama.
  • Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umaskini katika Mtaa.
  • Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote.
  • Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
  • NGAZI YA MSHAHARA
  • Ngazi ya Mshahara ni TGS B.

MAELEZO/MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Mwombaji awe Raia wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Barua ya maombi iambatanishwe na wasifu binafsi wa mwombaji wa hivi karibuni (Curriculum Vitae).
  • Maombi yaambatanishwe na nakala za vyeti vya elimu ya Kidato cha Nne/Sita, cheti cha kuzaliwa na vyeti vyote vilivyotajwa katika sifa za mwombaji.
  • “Testimonials” na “Professional Results” hazitakubaliwa.
  • Mwombaji aambatanishe picha mbili (Passport Size) za hivi karibuni katika barua yake ya maombi.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimefanyiwa uthibitisho na TCU na/au NACTE.
  • Waombaji ambao ni watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi kwa waajiri wao.
  • Mwombaji anatakiwa kuwa na kitambulisho cha Uraia (National Identification Card) au namba (National Identification Number) kwa ambao hawajapata vitambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
  • Maombi yawasilishwe kwa barua kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza.
  • Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 02 Mei, 2023 saa 9:30 Alasiri.

Barua za maombi zitumwe kwa kutumia anwani ifuatayo:-

Mkurugenzi wa Manispaa,

Halmashauri ya Manispaa ya Songea,

4 Barabara ya Sokoine,

S. L. P. 14,

57101 SONGEA – RUVUMA.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA:-

Dr. Frederick D. Sagamiko

MKURUGENZI WA MANISPAA

SONGEA

 

NB: Tangazo hili linafuta tangazo la kazi lenye Kumb.Na. SO/MC/L.10/7/IV/32 la tarehe 14 Aprili, 2023.    

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI RUVUMA

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma Awapongeza Wastaafu 86 wa Kada ya Ualimu Mkoani Ruvuma

    May 08, 2025
  • Kamati ya Siasa Wilaya Yaridhishwa na Hatua za Miradi ya Maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

YALIYOJIRI MAKABIDHIANO YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa