Majukumu ya Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto
1.Kuwezesha jamii kubuni mbinu shirikishi za kutelekeza,kusimamia na kutathimini mipango na miradi ya maendeleo.
2.Kuwezesha uhamasishaji wa jamii kwa njia ya mikutano na kuwapatia elimu elekezi juu ya umuhimu wa kushiriki na kuchangia shughuli za maendeleo.
3.Kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwajengea uwezo jamii na vikundi vya maendeleo.
4.Kuwezesha utoaji wa mafunzo ya kujengea uwezo mabaraza ya watoto kuanzia ngazi ya mitaa hadi Wilaya.
5.Kuyawezesha makundi maalum kwa kuyapatia mafunzo ya namna ya kuanzisha miradi,kuyasimamia na kuhakikisha uendelezaji unafanyika
6.Kuwaendeleza na kuwapatia elimu viongozi wa kisiasa wakiwemo madiwani ili waweze kupambana na ukatili wa kijinsia.
7.Kuvipatia taaluma vikundi vya ujasirimali vya wanawake na vijana ili waweze kubuni na kusimamia miradi yao iwe endelevu.
8.Kuwapatia watumishi wa Idara vitendeakazi sitahili ili waweze kufanikisha utekelezaji wa malengo ya Idara na serikali kwa ujumla.
9.Kuandaa na kutoa taarifa za Idara za robo na mwaka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa