Mwenyekiti wa Jumuiya za Tawala za Mitaa Tanzania ALAT Mkoa wa Ruvuma Kelvin Mapunda amewataka wajumbe wa ALAT kuendelea kuwa na ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya Serikali ili kufikia lengo linalokusudiwa.
Hayo yamejili katika ziara ya kutembelea miradi iliyofanyika kwa siku 2 kuanzia tarehe 07 hadi 08 Desemba 2022 Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma na kufanikiwa kukagua miradi mitatu ambayo ni ujenzi wa darasa 1 katika shule ya Sekondari masonya kwa gharama ya Mil. 20 fedha kutoka Serikali kuu, mradi wa ujenzi wa jengo la huduma ya dharula, jengo la WOD ya upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru iliyojengwa kwa Mil. 300 na kutembelea Makumbusho ya waliyokuwa wakiishi wapigania uhuru kutoka Msumbiji “ FRELIMO”.
Mhe. Mapunda alisema lengo kuu la kufanya ziara ni kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kujifunza na kujenga uhusiano bora baina ya viongozi wa Halmashauri moja hadi nyingine Mkoani Ruvuma.
Aliongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imefanya vizuri katika kusimamia miradi ya maendeleo kutokana na miradi hiyo kujengwa kwa kiwango bora na kukamilika kwa wakati. “Mwenyekiti aliwapongeza”.
Alitoa wito kwa Wataalamu wa Wilaya ya Tunduru kuhakikisha wanarekebisha changamoto ndogondogo zilizopo katika miradi iliyotembelewa pamoja na kutenga bajeti ya fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi ili majengo hayo yaweze kutumiwa na wananchi.
Kwa upande wa wajumbe wa ALAT Mkoa wa Ruvuma wameipongeza Serikali kwa kutunza makumbusho ya kihistoria ya Wapigania Uhuru kutoka Nchi jirani ya Msumbiji (FRELIMO) na kuwataka kulitunza eneo hilo na kulitangaza kwa lengo la kuwavutia watalii wa ndani na nje ya Nchi.
Walibainisha kuwa Serikali iangalie uwezekano wa kujenga na kuendeleza mahusiano na jamii ya Msumbiji ili shule na Taiifa kwa ujumla iweze kunufaika kitaalma kutoka kwa FRELIMO.
Naye Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana Masonya Makrina Ngonyani alisema shule ya sekondari Masonya ilipokea kiasi cha shilingi mil. 20 kwa ajili ya ujenzi wa darasa moja fedha kutoka Serikali kuu ambapo kwasasa ujenzi huo upo hatua ya ukamilishaji.
Pia Halmshauri ya Wilaya ya Tunduru ilipokea fedha kutoka Serikali kuu kupitia wahisani (IMF)
Kiasi cha shilingi cha mil. 300 kwaajili kujenga jengo la kitengo cha Huduma za dharula katika Hospitali ya Wilaya Tunduru kwa lengo la kutoa huduma bora za kitabibu kwa wananchi.
“Kikao hicho kimepangwa kufanyika mwezi februari 2023 ikiwa ni utekelezaji wa miongozo ya uendeshaji wa vikao vya ALAT kwa kila robo ya mwaka.”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
MWANDISHI WA ALAT MKOA WA RUVUMA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa