NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
21.09.2021
ALAT ni Jumuiya ya tawala za mitaa Tanzania ambayo iliundwa kikatiba mwaka 1984 Desemba na kuanza kutumika rasmi mwaka 1985 kwa lengo la kupigania haki za Halmashauri na kuwa sauti moja katika kuleta maendeleo ya Halmashauri husika pamoja na kufanya mawasiliano ya karibu na Serikali kuu.
Hayo yamebainishwa na Wakili wa Serikali ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Seligius Ngahi katika kikao maalum cha ALAT Mkoa wa Ruvuma ambacho kilihudhuriwa na Wakurugenzi wa Halmashauri 8, Wenyeviti wa Halmashauri 7, Meya 1 kutoka Manispaa ya Songea na uongozi ngazi ya Mkoa kilichofanyika leo tarehe 21 Septemba 2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa lengo la kujadili na kupitisha taarifa mbalimbali na kupeleka taarifa hizo kwenye kikao cha Jumuiya ya tawala za mitaa (ALAT) Taifa.
Ngahi alisema kwamba ALAT ni chombo kinachosaidia kukuza maendeleo ya Serikali za mitaa zilizo huru na kutoa mchango katika kupeleka madaraka kwa wananchi, kuwasaidia madiwani, Mameya na wenyeviti katika majukumu yao kama wawakilishi waliochaguliwa kidemokrasia pamoja na kutoa uongozi, kuhimiza, kukuza ufanisi, uhuru,uwajibikaji, uwazi na demokrasia kwenye mfumo wa Serikali za Mitaa Tanzania na kwingineko duniani.”Alibainisha”
Naye Katibu wa ALAT Mkoa wa Ruvuma Grace Quintine amewataka viongozi wote kutoa ushirikiano wakati wa kujadili changamoto za Halmashauri husika mara zinapojitokeza kupitia vikao vya ALAT ambavyo husaidia kutatua changamoto hizo.
Kwa upande wake Kelvin Mapunda ambaye ni Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Ruvuma ametoa rai kwa viongozi wa Halmashauri zote Mkoani Ruvuma kusimama imara na kutekeleza wajibu wao kwa lengo la kuleta maendeleo yenye tija kwenye Halmashauri zao.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa