Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kelvin Mapunda amewataka Viongozi na Wataalamu Mkoani Ruvuma kuhakikisha wanasimamia zoezi la utoaji wa chakula kwa wanafunzi shuleni.
Akizungumza na wazazi wa shule ya Msingi Maleta iliyopo kata ya Ndongosi Halmashauri ya Wilaya ya Songea wakati wa Ziara ya kamati ya ALAT ( Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania) kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi maendeleo ya Halamshauri ya Wilaya ya Songea.
Amepongeza wananchi wa kitongoji cha Maleta kwa kuweka Mkakati rafiki ambao unatekelezeka na wananchi hao kwa kuwa na mwitikio mkubwa wautoaji wa chakula kwa wanafunzi 327 wakiwemo wavulana 160 na wasichana 167. “Aliwapongeza”.
Mhe, Mapunda amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka Mpango Mkakati wa kuondoa changamoto ya uhaba wa miundombinu ya shule kwa shule za Msingi kupitia mradi wa BOOST ambao unatarajia kutekelezwa ifikapo mwaka wa fedha 2023/2024.
Aliongeza kuwa pamoja na Mkakati huo amewataka wananchi kuendelea kuwa na uzalendo wa kuchangia nguvu za wananchi wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kitongoji hicho.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mwl. Neema Maghembe alisema “ Ziara ya kamati ya ALAT Mkoa wa Ruvuma ilianza kwa kutembelea miradi ya maendeleo ikiwemo na ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu shule ya Msingi Maleta “Shikizi” ambayo ilijenhgwa kwa gharama ya shilingi Mil. 40 ikiwa nguvu za wananchi ni shilingi 3,260.000, Mfuko wa Jimbo tsh 2,000,000, ofisi ya Mkurugenzi kiasi cha Mil 16,000,000 fedha za mapato ya ndani pamoja na vifaa vya ujenzi. Mwl. Maghembe aliwashukuru.
Mwl Maghembe ametoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuwapatia fedha zaidi ya Bil 2 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya ikiwa ni miongoni mwa Halmashauri 8 Kitaifa zilizopewa fedha kwa ajili kujenga jengo la Wagonjwa wa TB na Ukoma.
Shule ya Msingi Maleta ipo katika kijiji cha Ndongosi katika kata ya Ndongosi ambayo ilianza kama shule shikizi yenye jumla ya wananfunzi 327.
Kwa upande wananchi kutoka katika kitonoji cha Maleta wakitoa shukrani zao kwa Serikali ambapo walisema “wamejipanga kuendelea kujitolea kutoa michango yao kwa lengo la kuendeleza shule hiyo.“
IMEANDALIWA NA,
AMINA PILLY
MWANDISHI ALAT MKOA WA RUVUMA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa