Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata Bakari Kawina ametangaza matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Mfaranyaki ambao ulikuwa na wagombea 6 kutoka vyama mbalimbali vya siasa ikiwemo na AAFP, ACT WAZALENDO, CCM, CUF, NCCR MAGEUZI, na UDP.
Uchaguzi huo umekuja mara baada ya kutokea kwa kifo cha aliyekuwa Diwani wa kata ya Mfaranyaki marehemu Ajira Kalinga ambaye alifariki tarehe 09 April 2023.
Akitangaza Matokeo hayo Msimamizi msaidizi ngazi ya kata alisema "jumla ya waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kata ya Mfaranyaki ni 6603 kati ya hao waliopiga kura ni 1985 , kura zilizokataliwa ni 17 , kura halali ni 1968, hivyo Mgombea Christopher Kayombo ametangazwa kuwa mshindi wa Udiwani katika kata ya Mfaranyaki ."
Ushindi huo umetangazwa leo tarehe 19 Septemba 2023 katika ukumbi wa ofisi ya kata ya Mfaranyaki kwa kushirikisha wahusika wanaoruhusiwa kuwepo wakati wa kujumlisha kura.
Aidha, uchaguzi huo ulikuwa na wagombea 6 ambao ni Mgombea Mohamed Sandali Sony kutoka chama cha AAFP amepata kura 06 , Mohamed Selemani Haule - ACT WAZALENDO amepata kura 76 , Christopher Fabian Kayombo - CCM amepata kura 1872, Ahamad Alon Mambo - CUF amepata kura 10 , Pius Luoga Samola - NCCR MAGEUZI amepata kura 03, pamoja na mgombea Nasibu Selemani Haule – UDP amepata kura 01.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa