HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii inaendelea kuratibu na kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo na utoaji wa mikopo ya asilimia 10% kwa wanawake 4%, vijana 4% na walemavu 2% kwa mwaka 2021/2022 Tshs milioni 465 zilitolewa kwa lengo la uwekezaji na kiuchumi kwa vikundi.
Ili kufikia lengo lililokusudiiwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea imetenga maeneo rasmi ya uwekezaji wa viwanda kwa vikundi 11 vya ushonaji, kiwanda cha utengenezaji wa batiki, kiwanda cha uchakataji maziwa, kiwanda cha Welding na Aluminium, kiwanda cha uchakataji wa mazao ya nyuki pamoja na kiwanda cha uchakataji wa mafuta ya alizeti.
Utekelezaji wa ujenzi wa viwanda vidogo kata ya Lilambo ulishakamilika sambamba na ununuzi wa vitendea kazi kwa kila kiwanda tajwa na hatimaye uwekezaji wa vikundi kiuchumi umeanza kufanya kazi katika nyanja mbalimbali.
Mhandisi Fredrick Mbawala amesema amepokea mashine ya kukamua mafuta ya alizeti na karanga iliyonunuliwa kwa gharama ya shilingi Mil. 36,300,000 ambayo ameanza kuifunga kwa ajili ya kikundi cha Tumaini ambapo alibainisha kuwa “ Mashine hiyo ni bora na ya kisasa kwasababu inauwezo wa kukamua, kuchemsha, na kuchuja mafuta ya alizeti Tan 6.5 kwa siku ambapo mara baada ya kukamilisha kufunga mashine ukamuaji wa mafuta utaanza hivi karibuni. “Alibainisha”
Bi Halima Mango ni miongoni mwa wanakikundi cha Tumaini alianza kwa kutoa pongezi kwa Serikali kwa kuwakopesha kiasi cha fedha mil. 70 ambazo zimetumika kujenga jengo na kununua mashine ambayo itatumika kwa ajili ya kukamua mafuta ya alizeti na karanga. “ alipongeza”
AMINA PILLY,
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa