Hifadhi ya Taifa ya Saanane iliyopo jijini Mwanza, ilianzishwa kama bustani ya kwanza ya wanyama nchini mwaka 1964. Lengo la kuanzishwa kwake ilikuwa kuhamasisha uhifadhi na kuelimisha jamii.
Jina la hifadhi hii lililokana na mwanzilishi wa bustani aliyeitwa Saanane Chawandi ambapo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alinunua ardhi hiyo toka kwa mzee Saanane kwa shilingi 600 mwaka 1964..
Kati ya mwaka 1964 na 1966 wanyama mbalimbali walihamishiwa katika kisiwa hiki.
Wanyama hao ni pamoja na, digidigi, tembo, pofu, pundamilia, pongo, swala pala, ngiri, kima, twiga, nungunungu, mamba n.k
Wanyama wakali kama simba wamefungiwa na wanyama wapole waliachwa huru.
Bustani hii iligeuzwa kuwa pori la akiba (game reserve) mwaka 1991.
Muonekano wa Ziwa Victoria kutoka katika kisiwa cha Saanane ni kivutio kikubwa. Vilevile muonekano wa Kisiwa cha Saanane uwapo jijini Mwanza ni kivutio kingine kikubwa.
Hifadhi hii ina eneo la kilomita za mraba 0.5, na iko umbali wa km 2 kusini magharibi kutoka katikati ya jiji la Mwanza, katika Ghuba ya Ziwa Victoria.
Kisiwa cha Saanane kinafikika kwa boti ukiwa Mwanza. Mtu anaweza kufika Mwanza kwa gari, ndege ama treni na kutoka Mwanza mjini kutembea kwa miguu ama kwa gari hadi geti la kuingilia Hifadhini.
Shughuli za kufanya hifadhini Saanane ni pamoja na kuangalia wanyama, kukwea miamba, kutizama ndege, na safari za kutembea.Vilevile, kupiga makasia kwa kutumia boti za wenyeji inaruhusiwa kupitia kwa mawakala wa utalii.
Hifadhi hii inafikika wakati wowote wa mwaka.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa