MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema Mkandarasi anayejenga barabara ya lami toka Mbinga hadi Mbambabay wilayani Nyasa anaanza ujenzi mwezi huu ambapo TANROAD mkoa wa Ruvuma wamempokea Mkandarasi huyo tangu Ijumaa iliyopita akiwa na mitambo ya kufanyiakazi.
Ujenzi wa barabara ya lami katika kiwango cha lami nzito,unaanza mara moja ambapo serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 67 toka Mbinga hadi Mbambabay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ambayo itagharimu shilingi bilioni 129.
Mkataba huo wa miezi 36 umesainiwa Desemba 11,2017 na Kampuni ya Mkandarasi inayoitwa China Henan International Corparation Group Ltd(CHICO) ambayo inatarajia kukamilisha kazi ya ujenzi wa barabara hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020.
Kukamilika kwa kipande cha barabara toka Mbinga hadi Nyasa kunakamilisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami katika ukanda wa Mtwara Corridor toka Mtwara hadi Mbambabay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma hivyo kufungua milango ya uwekezaji katika ukanda wa kusini.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa