Mradi wa kituo cha Mabasi Tanga uliojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 6.8 wenye lengo mahususi la kufanya uwekezaji wa mradi kwa msingi na matumizi sahihi ya stendi ili iweze kutumika kwa kiwango tarajiwa na kupata faida iliyokusudiwa na Serikali pamoja na jamii ya Manispaa ya Songea.
Tamko hilo limetolewa na Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Leodgar Mbano akiwa katika baraza maalmu la madiwani wa Manispaa ya Songea lililofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea 29 disemba 2020.
Mbano, ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la Madiwani Manispaa ya Songea alisema lengo la kikao hicho ni kupitisha mapendekezo ya kuhamia stendi kuu ya Songea iliyopo shule ya Tanga ifikapo 01 januari 2020 ambalo ni utekelezaji wa maelekezo ya Mh. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ikifuatiwa na agizo la Mh. Waziri Selemani Jafo akiwa ziarani Mkoani Ruvuma 23 disemba mwaka huu ambapo miongoni mwa miradi aliyotembelea ni pamoja na kituo kikuu cha mabasi Tanga.
Awali katika kutekeleza maagizo hayo aliitisha kikao cha wadau wa umiliki wa vyombo vya usafirishaji abiria, vongozi wa wasafirishaji abiria (UWARU), Pamoja na Afisa usalama barabarani Mkoa wa Ruvuma, Afisa mfawidhi wa LATRA, Meneja wa TARURA pamoja na wadau wengineo kwa lengo la kuwashirikisha katika matumizi sahihi ya Stendi. “ Alisisitiza Mbano”.
Naye Mchumi Manispaa ya Songea Andambike B. Kyomo alisema “ Halmashauri imeleta mapendekezo hayo kwa mabasi yote yanayokwenda dar es- salaam, njombe, Iringa, Mbeya, Sumbawanga, Dodoma kupitia barabara ya Njombe safari zao zitaanzia na kuishia stendi kuu ya Tanga na wote wanatakiwa kushuka stendi ya Tanga.
Kyomo aliongeza kuwa Mabasi yote yanayofanya safari zake kupitia barabara ya Lindi kwenda dar es- salaam, lindi, Mtwara, Tunduru na Masasi yataanzia na kumalizia safari zake stendi kuu ya Tanga isipokuwa yatakuwa yanapakia na kushusha abiria kwa dakika tano 5 tu katika Stendi ya Seedfarm kwa muda, wakati inapoandaliwa barabara ya kuunganisha Mletele na stendi ya Tanga.
Pia Mabasi yote yanayoelekea Mbinga, Nyasa, na Songea Vijijini safari zake zitaanzia na kumalizia Stendi ya Tanga, yanapokwenda na kurudi yatatakiwa kupita barabara ya Bombambili-Matarawe hadi mwembechai na yataruhusiwa kushusha na kupakia stendi ya Ruhuwiko.
Aidha, magari yanayoanzia safari zake makambako, Njombe, Mavanga, Mateteleka, Wino, Ifinga na madaba safari zao kuishia stendi ya Tanga na kuondokea stendi ya Tanga. Pia mabasi yote yanayokwenda nje ya Mkoa yataanza safari saa 12.00 asubuhi na yanatakiwa kuwepo stendi ya Tanga saa 11: 00 alfajiri kila siku kwa ajili ya kurahisisha kukaguliwa na kikosi cha usalama barabarani.
Daladala za Mletele zitamalizia safari zake stendi ya daladala Mfaranyaki, pia Magari yanayokwenda Peramiho yataanza safari zake stendi kuu ya Tanga kupitia stendi ya Mfaranyaki kwa dakika tano tu, pia ukomo wa daladala zote za Mshangano utakuwa stendi kuu ya Tanga.
Alisema ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii ndani ya stendi tunahamasisha wafanyabiashara ili waweze kuwekeza katika maeneo hayo ili huduma ziweze kupatikana muda wote.
Akizitaja faida zitakazopatikana baada ya mabadiliko hayo ni matarajio ya makusanyo ni jumla ya shilingi 580,500,000/= ikilinganishwa na mapato ya sasa ambayo ni 165,780,00/=. Umetolewa Wito kwa vyombo vya usalama kuhakikisha wananchi wanafika stendi kuu ya Tanga kwa usalama nyakati za usiku na alfajiri.
Baada ya kusema hayo, baraza la madiwani likiongozwa na Mwenyekiti wa baraza hilo walisema” wamekubali mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu na wamekubaliana kwa pamoja kubadilisha matumizi ya Stendi ya Msamala kuwa soko la Mazao ya nafaka.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANBISPAA YA SONGEA.
30 disemba 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa