Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewataka Wataalamu wote kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuikamilisha kwa wakati kabla ya tarehe 30 juni 2023.
Amesema kila kiongozi anatakiwa kuwajibika katika eneo lake kwa kuishirikisha jamii husika ili kutatua changamoto za wananchi ikiwemo na miundombinu ya shule, Afya na Barabara kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita.
Alibainisha kuwa, katika kipindi cha robo ya kwanza Manispaa ya Songea ilipokea zaidi ya Bil. 1.5 pia katika kipindi cha robo ya pili na ya tatu Manispaa ya Songea imepokea Bil. 1.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Alipongeza”.
Mhe. Mbano amewataka Madiwani wote kutembelea kata ya Matogoro kujifunza namna walivyoweza kufanikisha kutatua changamoto za madawati kwa shule za msingi na Sekondari kwa lengo la kuondoa changamoto mbalimbali za wananchi “. Alisisitiza.”
Ametoa wito kwa wataalamu kuhakikisha wanaongeza bidii ya ukusanyaji wa mapato ya ndani, utoaji wa chakula kwa wananfunzi shuleni, pamoja na usafi wa mazingira.” Mhe. Mbano alibainisha.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Komredi Mwinyi Msolomi amewataka Wataalamu kusimamia usafi wamazingira hususani katika maeneo ya Soko, na makazi ya watu.
Naye katibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini James Mgego ametoa wito kwa watumishi na Madiwani kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo na kuongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kufikia lengo lililokusudiwa na Serikali.
IMEANDALIWA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa