Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewataka wakuu wa Idara na Vitengo kuendelea kusimamia miradi Viporo yote na kukamilisha ifikapo tarehe 01 Oktoba 2022 kabla ya kuanza kwa ujenzi wa miradi mipya ya madarasa ambayo yanatakiwa kuanza kujengwa hivi karibuni kwa ikiwa ni maandalizi ya kupokea wananfunzi wa kidato cha kwanza 2023.
Kauli hiyo imetamkwa leo 28 Septemba 2022 katika baraza la Madiwani la Halmashauri kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya hesabu za mwaka 2021 hadi 2022 ambalo ni utekelezaji wa sheria ya Serikali za Mitaa ya 1982 kifungu na.40 kama ilivyorekebishwa mwaka 2000 ambayo imeeleza bayana kuwa “Halmashauri nchini zinapaswa kufunga hesabu na kuwasilisha kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) si zaidi ya tarehe 30 Septemba ya kila mwaka. “
Mbano alieleza kuwa Swala la Hoja sio la Mweka Hazina pekee bali ni la kila Mkuu wa idara anatakiwa ahakikishe Idara yake inaleta majibu ya Hoja inayomhusu ili Taasisi iweze kuwa na mwendelezo wa kupata Hati Safi, Hivyo amewataka wataalamu hao kujibu hoja zote kwa usahihi na kukamilisha ifikapo 01 Oktoba 2022 hoja zote ziwe zimejibiwa. Alisisitiza.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema amewataka Wataalamu mara baada ya kufunguka kwa mfumo wa malipo wahakikishe wanasimamia miradi ambayo ilikuwa haiendelezwi kutokana na tatizo la mfumo wa malipo kutofunguka kwa wakati.
Pololet amewaagiza wataalamu kuwa wahakikishe wanatekeleza na kukamilisha Miradi yote ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, kituo cha afya Lilambo, Kituo cha afya Mletele, ujenzi wa mabweni na madarasa shule ya wavulana na wasichana Songea inakamilika mapema iwezekanavyo.
Naye kaimu Mweka Hazina Manispaa ya Songea Mustafa Matili amesema kuwa uundaji wa hesabu kuishia 30 juni 2020 umezingatia sheria za fedha, sheria ya manunuzi ya mwaka 2011, sheria ya fedha za Serikali za mitaa ya mwaka 1982 kama ilivyorerekebishwa mwaka 2000, pamoja na miongozo inayotolewa na bodi ya uhasibu, Sera za Nchi na Halmshauri ya Manispaa ya Songea.
Matili aliongeza kuwa Fedha taslimu imeongezeka kutoka shilingi 1,299,046,043 mwaka 2021 hadi shilingi 1,702,294,995 kwa mwaka 2022 ambayo imetokana na fedha za ujenzi wa vituo vya afya ambazo zilipokelewa mwishoni mwa mwaka.
IMEANDALIWA NA
AMINA PILLY.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa