VIJANA 53 wa Mkoa wa Ruvuma, wamepewa vyeti vya mafunzo ya ujasiriamali ambayo yamefundishwa ndani ya siku tatu watalaam wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC), ambalo lipo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu(kazi,vijana,Ajira na wenye ulemavu).
Akizungumza baada ya kukabidhi vyeti hivyo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea, Afisa Maendeleo ya Vijana Mwandamizi wa OWM-KVAU Godfrey Massawe amesema vijana wengi wamejiingiza kwenye biashara ila hawana elimu ya kuweza kuendeleza biashara.
Amesema hali hiyo imesababisha NEEC kuanza kufundisha elimu ya kujitambua kwa mjasiriamali,pia vijana hao wameunganishwa na fursa mbalimbali za uwezeshwaji katika biashara zao.
Massawe ameyataja malengo ya kuwakutanisha vijana na Taasisi ambazo wanaweza kukutana nazo ili kuweza kufanya kazi nao na kutatua changamoto zao katika matatizo ya mtaji, namna ya kuweza kukuza biashara na kupata vifaa vya kutumia katika kazi zao.
“Tunafanya kazi kwa ukaribu na secretary ya Mkoa, maafisa biashara, tunao waratibu wa dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi katika ngazi za Mkoa na Halmashauri, wao ndio wamewabaini hawa vijana wanaohitaji haya mafunzo tunawapa majukumu ya kuweza kuwafuatilia baada ya miezi mitatu katika biashara zao ili kujua kile tulichofundisha wamepiga hatua gani’’,alisisitiza Massawe.
Janeth Otilia ni mmoja wa wajasirimali wadogo aliyebahatika kushiriki katika mafunzo hayo,ameipongeza serikali kwa kugharamia mafunzo hayo,ambayo amesema yatasaidia kufungua fursa mpya za kibiashara hivyo kufanya biashara zenye tija na ufanisi wa hali ya juu na kwamba yupo tayari kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenzake ambao hawakupata fursa hiyo.
Hata hivuyo Otilia ameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu ya ujasirimali na biashara hadi vijijini ili kuweza kuwasaidia vijana wa vijijini kuondokana na changamoto ya ajira na mimba za utotoni.
Naye,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Matogoro stick industry a Richard Greyson amesema atajitahidi kutoa elimu kwa wajasiriamali wenzake ili kupata faida ambayo amepata na kutumia fursa ambao wamefundishwa kutoka Taasisi mbalimbali zikiwemo TRA,TBC,OSHA na PASS.
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa nane hapa nchini ambayo imepata fursa ya vijana kufundishwa program ya ujasirimali na biashara ambapo mafunzo hayo yanatarajia kunufaisha vijana 153 kutoka katika Mkoa wa Ruvuma.
Imeandikwa na Farida Mussa
Wa Kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 12,2019.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa