TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Hali ya upatikanaji wa mbolea katika Mkoa wa Ruvuma
Katika msimu wa kilimo 2019/2020 wakulima wameitikia kilimo kwa kuongeza ukubwa wa mashamba na kutumia teknolojia pamoja na mbinu za kilimo bora. Hali hii imechochewa na bei nzuri ya mazao ya msimu 2018/2019. Mbolea nyingine zimeendelea kupatikana isipokuwa UREA imeonekana kuhitajika kwa wingi.
Upungufu wa mbolea ya UREA
Katika msimu huu wa 2019/2020 kumekuwa na ongezeko la matumizi ya mbolea za kukuzia aina ya UREA. Juhudi kubwa za ufumbuzi zimefanwa na Serikali kwa kuingiza meli za mbolea kwa awamu tofauti. Meli ya kwanza ilishusha tani elfu 10 mwezi Januari 2020 ambazo zilisambazwa kwa wakulima na meli ya pili inaendelea kushusha jumla tani elfu 43 katika bandari ya Dar es salam ambazo ambazo zitafika kwa wakulima mwanzoni mwa mwezi Februari 2020.
Wafanyabiashara wa mbolea wa Mkoa wa Ruvuma wanaaswa kwenda Dar es salaam kuchukua mbolea na kuzisambaza kwa wakulima kwa kuzingatia sheria kanuni na miongozo.
Matumizi ya mbolea mbadala
Mkulima anashauriwa kutumia mbolea mdadala kukuzia mazao yake endapo mbolea ya UREA itakuwa haipo sokoni. Mbolea hizo ni SA, CAN, Minjingu Top-Up, YARA Cereal, YARA Amidas na YARA Sulfan.
Usimamizi wa bei elekezi za mbolea
Mkoa wa Ruvuma na halmashauri zake umepewa jukumu la kusimamia mwenendo wa bei za mbolea kwa mujibu wa sheria ya mbolea ya mwaka 2009 na kanuni zake kama zilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2011 na 2017.
Mbolea zinazohusika katika manunuzi ya mbolea kwa pamoja (BPS) ni UREA na DAP. Bei hupangwa kwa kuzingatia umbali wa maeneo ya pembezoni kama majedwali yanavyoonekana;
(i). Bei elekezi za mbolea UREA Msimu 2019/2020
Na
|
Halmashauri
|
Bei ya rejareja (TSh) - mkulima |
Bei ya jumla (TSh) - mfanyabiashara |
1 |
MADABA (Mtyangimbole)
|
55,195 |
52,663 |
2 |
MBINGA DC (Muungano)
|
56,424 |
53,836 |
3 |
MBINGA TC (Kihungu)
|
55,854 |
53292 |
4 |
NATUMBO DC (Magazini)
|
56,364 |
53,778 |
5 |
NYASA DC (Mipotopoto)
|
56,844 |
54,236 |
6 |
SONGEA DC (Lilahi)
|
55,531 |
52,983 |
7 |
SONGEA MC (Mwengemshindo)
|
55,195 |
52,663 |
8 |
TUNDURU (Kalulu Via Lindi)
|
54,775 |
52,263 |
(ii). Bei elekezi za mbolea DAP MSIMU 2019/2020
Na |
Halmashauri |
Bei ya rejareja (TSh) |
Bei ya jumla (TSh) |
1 |
MADABA (Mtyangimbole)
|
59,663 |
56,348 |
2 |
MBINGA DC (Muungano)
|
60,881 |
57,498 |
3 |
MBINGA TC (Kihungu)
|
60,316 |
56,965 |
4 |
NATUMBO DC (Magazini)
|
60,821 |
57,442 |
5 |
NYASA DC (Mipotopoto)
|
61,296 |
57,891 |
6 |
SONGEA DC (Lilahi)
|
59,996 |
56,662 |
7 |
SONGEA MC (Mwengemshindo)
|
59,663 |
56,348 |
8 |
TUNDURU (Kalulu Via Lindi)
|
59,247 |
55,956 |
Kufungua mifuko
Kumetokea tabia ya watu kufungua na kuuza kwa kupima mbolea kwa watumiaji wadogo ya mazao ya bustani. Hairuhusiwi kufungua mifuko ya mbolea na kuipima kwani inaharibu ubora wa mbolea. Mbolea hupoteza ubora kupitia mvuke na kubaki makapi mabayo hayafai kwa mmea.
Hilo ni kosa na atakayebainika itampasa kupelekwa kwenye vyombo vya sheria ili apate adhabu ya kufungwa au kulipa faini kwa mujibu wa sheria.
Onesmo Kenani Ngao
AFISA KILIMO – RS RUVUMA
29/01/2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa