WAWAKILISHI wa Benki ya Dunia ambayo imefadhili miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa bustani ya Manispaa hiyo na kuridhishwa na kiwango cha ujenzi wake.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imepokea jumla ya sh.milioni 400 kwa ajili ya uboreshaji wa Bustani ya Manispaa ya Songea.
Mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya Mpango wa Kuzijengea uwezo serikali za mitaa(ULGSP) unatarajiwa kugharimu sh.milioni 399.95.
Mradi huo uliopo mkabala ya Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Songea una eneo la mgahawa,choo cha kulipia,uzio na maeneo ya kupaki magari(parking bay).
Bustani hiyo ya aina yake katika mji wa Songea ina eneo la kupumzikia(resting huts) na maeneo ya kuchezea watoto.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa