BENKI ya Dunia imetoa zaidi ya sh.bilioni 27 katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inachangia kukuza uchumi wa manispaa hiyo.Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Tina Sekambo Akizungumza ofisini kwake mjini Songea jopo la wanahabari walioongozwa na Kitengo cha mawasiliano cha TAMISEMI ametaja miradi ambayo imefadhiliwa na Benki ya Dunia kuwa ni ukarabati wa barabara za lami nzito zenye urefu wa kilometa 10.3 zilizogharimu zaidi ya sh.bilioni 10 na ujenzi wa Stendi mpya ya kisasa katika eneo la Kata ya Tanga ambao awamu ya kwanza inagharimu shilingi bilioni sita.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo miradi mingine ni ujenzi wa machinjio ya kisasa katika eneo la Kata ya Tanga ambao umegharimu shilingi bilioni 3.2,ujenzi wa bustani ya kisasa ya Manispaa ya Songea uliogharimu zaidi ya sh.milioni 399 na ukarabati wa Stendi ndogo katika eneo la Kata ya Mfaranyaki ambao umegharimu zaidi ya sh.bilioni tatu. Amesema miradi yote ikikamilika itachochea uchumi wa manispaa hiyo na kuongeza ajira na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Hata hivyo ili miradi yote iwe endelevu ametoa rai kwa wananchi wa Manispaa hiyo kuilinda miradi hiyo na kuwa ficus wote ambao watafanya hujuma ya aina yoyote ikiwemo kuharibu miundombinu ya miradi hiyo ambayo imegharimu mabilioni ya fedha. Manispaa ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri 18 nchini za miji na manispaa zinazotekeleza mpango wa kukuza uchumi wa Halmashauri hizo kupitia Benki ya Dunia.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari wa manispaa ya Songea
Mei 29,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa