BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya afya vyenye thamani ya shilingi milioni tano katika kituo cha Afya cha Madaba kilichopo katika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo katika hafla ambayo imefanyika katika Kituo cha Afya mjini Madaba,Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Janeth Shango amevitaja vifaa vilivyotolewa kuwa ni vitanda vitano na magodoro yake kulalia wagonjwa,kitanda kimoja cha kujifungulia akinamama na mashuka 50.
“Katika kipindi cha mwaka 2018,Benki ya NMB imeweza kuchangia huduma za afya na elimu zaidi ya shilingi bilioni moja,kwa hiyo unaweza kuona ni namna gani NMB ipo karibu na jamii’’,alisema Shango.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema ambaye ameipongeza Benki ya NMB kwa kuonesha kwa vitendo kuwa ipo karibu na jamii baada ya kutoa msaada wa vifaa hivyo na kutoa rai kwa watanzania kuiunga mkono Benki hiyo.
“NMB inatoa huduma karibu zote,kwa watu wazima na watoto,pia tunapata huduma kupitia mitandao ya simu za mkononi, tunaweza kufanya biashara kwa kuwa mawakala wa Benki’na huduma nyingine’,alisisitiza Mgema.
Amesema Benki hiyo inaunga mkono kuboresha afya za wananchi ambapo,imetoa msaada wa vitanda,magodoro na mashuka na kwamba kitendo hicho kinaonesha kuwa NMB inawatakia watanzania maisha marefu na ameahidi serikali katika Wilaya ya Songea itaendelea kuiunga mkono Benki hiyo ili iweze kufanya biashara kwa ufanisi.
Mgema ameipongeza NMB kwa kufungua tawi la Benki hiyo katika Halmashauri ya Madaba ambayo ipo umbali wa kilometa 120 kutoka mjini Songea.
Hata hivyo amesema Halmashauri hiyo ambayo imeanza miaka mitatu iliyopita hivi sasa ina watumishi wa umma zaidi ya 500 ambao wanatakiwa kufungua akaunti za kupitishia mishahara yao kila mwezi katika Benki.
“Kwa watumishi hawa wa Madaba kwa vyovyote vile ni lazima wafungue akaunti zao katika Benki ya NMB tawi la Madaba kwa sababu ndiyo Benki Pekee iliyo karibu yao’’,alisema.
Akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo,Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Madaba Janeth Makoye,amesema kabla ya msaada huo,Kituo cha Afya Madaba kilikuwa na vitanda 24 vya kulala wagonjwa na vitanda vitatu tu vya kujifungulia akimama ambao walipewa na Rais.
“Hivi sasa tuna upungufu wa vitanda vya kujifungulia akinamama vinne,NMB mlio karibu yetu mmeonesha mfano wa kuigwa na Taasisi na wadau wengine
BENKI ya NMB ndiyo inayoongoza nchini ikiwa na wateja milioni tatu,matawi 228 ambayo yameenea katika nchi nzima,ikiwa na mashine za kutolea fedha (ATM) zaidi ya 800.
Imeandikwa na Albano Midelo
Novemba 8,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa