Kwa upande mwingine, shilingi 1,500,000,000 zinazotokana na fedha za jimbo na tozo ya mafuta zitatumika kujenga barabara zenye urefu wa kilomita 24.15 kwa kiwango cha changarawe, pamoja na kilomita 1 kwa kiwango cha lami.
Pia, fedha hizo zitatumika kujenga boksi kalvati 4 ili kuboresha miundombinu na kurahisisha usafiri katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Songea
Aidha, katika kipindi cha mwaka 2025/2026 Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Manispaa ya Songea ilitengwa bajeti ya shilingi 2,597,600,000, kwa ajili ya matengenezo na ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Akizungumza Mhandisi Dotto Magesa kwa niaba ya Meneja TARURA Manispaa ya Songea wakati wakuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TARURA kwa mwaka wa fedha 2025/26 katika baraza la Madiwani manispaa ya songea, Meneja wa TARURA Wilaya ya Songea, Alisema fedha hizo zimetokana na fedha za matengenezo, mfuko wa jimbo pamoja na tozo mbalimbali.
Mhandisi Magesa aliongeza kuwa " mtandao wa barabara unaohudumiwa na TARURA katika Manispaa ya Songea una jumla ya kilomita 513.65, ambapo kilomita 256.420 ni barabara za mjazo, kilomita 255.160 ni za mkusanyo na kilomita 2.070 ni za jamii."
Ameeleza kuwa kati ya mtandao huo, kilomita 43.46 ni za lami, kilomita 75.67 ni za changarawe huku kilomita 394.52 zikiwa ni barabara za udongo.
Aidha, amesema Manispaa ya Songea ina jumla ya taa za barabarani 393, hatua inayosaidia kuimarisha usalama na mwonekano wa barabara nyakati za usiku.
Katika tathmini ya hali ya barabara, Mhandisi Bakari amesema asilimia 73.54 ya barabara zipo kwenye hali nzuri, asilimia 24
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa