Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kutoa kiasi cha fedha Bil. 3.12 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Mkoani Ruvuma.
Kanal Laban ametoa shukrani hizo katika kikao kazi cha Mkoa wa Ruvuma chenye lengo Mahususi katika kutoa taarifa yamapokezi ya fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa 156 katika shule za Sekondari kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea 04 Oktoba 2022 na kuhudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama Mkoa, Wakuu wa Wilaya zote, Wakurugenzi na Wataalamu mbalimbali.
Alisema kuwa Lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha inaondoa tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari ambao utasaidia kuwaondolea kero wanafunzi, wazazi au walimu na kuwezesha kuwa na mazingira bora na rafiki kwa wanafunzi.
Amewataka viongozi wote Mkoani Ruvuma kutoa ushirikiano katika kutekeleza na kusimamia miradi hiyo kwa kuzingatia taratibu za ujenzi ili kufikia lengo lililowekwa na kuhakikisha mradi unakamilika kabla ya tarehe 05 Disemba 2022.
Alibainisha kuwa Mwaka 2021/2022 Mkoa wa Ruvuma ulipokea Bil. 10 kupitia mradi UVIKO 19 ambao uliwezesha kujenga vyumba vya madarasa 500 kwa shule za Msingi na Sekondari ambao ulishakamilisha pia kupitia mradi wa Mpango wa boresha elimu, Mkoa wa Ruvuma ulipokea Bil. 7.7 kwa ajili ya ujenzi wa shule 10 za Sekondari ambao ulitakiwa ukamilike kufikia tarehe 30 Septemba 2022, hivyo ametoa rai kwa Halmashauri ambazo bado hazija kamilisha ujenzi kukamilisha haraka iwezekanavyo.
Ameagiza Wilaya zote kufanya vikao vya mitaa na vijiji ili kutambulisha mradi kwa wananchi kwa lengo la kuleta ushirikishwaji na uwajibikaji kwa jamii pamoja na kuunda kamati za miradi, kufuata B.O.Q za mradi husika, pamoja na ununuzi wa vifaa vya ujenzi ufuate mchakato wa manunuzi. “Kanal Laban alisisitiza.”
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoani Ruvuma Jumanne Mwankhoo alisema kila maradi unatakiwa utekelezwe kwa kufuata maelekezo ikiwemo na kutumia Mfumo wa FORCE ACCOUNT, kuzingatia ramani ya mradi husika, kuweka uwazi wakati wa kutangaza nafasi za kazi na kuweka kwenye TOVUTI za Mikoa na Halmashauri na mbao zote za Halmashauri, ujenzi wa vyumba vya madarasa uendane na utengenezaji wa madawati 50 na meza 50, mradi uendane na thamani ya fedha, na kutumia uzoefu uliotumika wakati wa utekelezaji wa mradi wa UVIKO 19.
Mwankhoo aliongeza Fedha za mradi zimeshaingizwa katika shule 68 Mkoani Ruvuma ambapo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepokea kiasi cha shilingi Bil. 1.52 ambazo zitatumika katika ujenzi wa vyumba vya madarsa 76.
Naye mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho amewataka watalamu na viongozi mbalimbali Mkoani Ruvuma kutoa ushirikiano katika kutekeleza mradi ili kufikia lengo lililowekwa na Serikali.
AMINA PILLY.
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa