MBUNGE wa Jimbo la Songea mjini Dk.Damas Ndumbaro ametoa rai kwa watanzania hususani wakazi wa Jimbo lake kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi wanyonge.
Amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Chama Tawala CCM,imekuwa inafanya miradi mikubwa inayowanufaisha watanzania wengi ukiwemo mradi wa umeme wa Grid ya Taifa toka Makambako hadi Songea uliogharimu bilioni 208 ambao unatarajia kukamilika Agosti mwaka huu na kuwashwa Manispaa ya Songea Septemba mwaka huu.
Amesema baadhi ya majarida ya barani Ulaya hususani katika nchi ya Ufaransa yamemwandika Rais Magufuli kuwa ni tofauti na Marais wengi wa Afrika ambao wamekuwa wanayatumikia zaidi Mataifa tajiri ya nje badala ya wananchi wao.
Tangu uhuru mji wa Songea haujaunganishwa na umeme wa Grid ya Taifa badala yake Shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO mkoa wa Ruvuma wamekuwa wanatumia umeme wa genereta ambao sio wa uhakika na kuaminika.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa