• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BILIONI 216 zatumika kukamilisha mradi wa umeme wa Grid Makambako-Songea

Tarehe ya kuwekwa: September 14th, 2018

MRADI wa Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme toka Makambako mkoani Njombe hadi Songea mkoani Ruvuma ambao umegharimu shilingi bilioni 216  umekamilika kwa asilimia 100 .

Waziri wa Nishati Dkt.Merdad Kelamani amesema utekelezaji wa mradi huu ulianza Septemba 2016 na kukamilika Septemba 2018 na kwamba mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi

Dkt.Kelamani amesema sehemu ya kwanza ya mradi huu imehusisha ujenzi wa vituo vitatu vya kufua umeme mkubwa wa kilowatts 220 vilivyojengwa Makambako, Madaba na Songea na kwamba Sehemu ya pili ya mradi imehusisha ujenzi wa miundombinu ya kusafirishia umeme unaofuliwa katika vituo hivyo vitatu

“Sehemu ya tatu ya mradi ni kusambaza umeme katika vijiji 122 vya mikoa miwili ya Njombe na Ruvuma,Mradi wa Umeme Makambako-Songea utaunganisha wateja wa awali wapatao 22,700 na kadri unavyoendelea wananchi wengi zaidi wataendelea kuunganishwa’’,anasisitiza Dkt.Kalemani.

Amesema mradi huo ambao  umegharimu shilingi bilioni 216 ambazo zimetolewa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Swedeni na  mradi huu unatarajiwa utafunguliwa rasmi mwisho wa mwezi huu wa Septemba

Hata hivyo amesema Ifikapo Septemba 26 mwaka huu itawashwa mitambo na wananchi wataanza rasmi kutumia umeme kutoka kwenye mradi huu wa Makambako-Songea

Amesema mradi huu utakuwa na manufaa makubwa ikiwemo wananchi kuunganishiwa umeme kwa bei nafuu ya mradi wa REA ya shilingi elfu 27

“Tukiwasha mitambo ya mradi huu tutazima rasmi mitambo ya umeme iliyokuwa inatumia mafuta mazito iliyoko Madaba, Ludewa, Mbinga, Namtumbo na Songea Mjini’’,anasisitiza Waziri wa Nishati.

Amesema Mitambo ya umeme inayotumia mafuta mazito ilikuwa inagharimu shilingi bilioni 1.9 kwa mwaka.Ametoa wito kwa wananchi watumie umeme huu mkubwa kwa ajili ya kujenga uchumi wa viwanda

Kulingana na Dkt.Kalemani hadi sasa kuna jumla ya Megawatts 1568 kwenye gridi ya taifa na kwamba matarajio ni  kuunganisha umeme kwenye vijiji 5100 nchini ambapo kuanzia Julai hadi Septemba 2018 tayari vijiji 818 vimeshaunganishwa

“Ifikapo Juni 2021 vijiji vyote 12,268 vya Tanzania vitakuwa vimeunganishiwa umeme,Mradi wa kuzalisha megawatts 600 za umeme wa makaa ya mawe utaanza Julai 2019,Kuanzia tarehe 15 Septemba 2018 tumetangaza kuwa wawekezaji wenye nia na uwezo wa kuzalisha umeme wa upepo na jua waje kuanza uzalishaji’’,anasema.

Hata hivyo amesema Miaka miwili ijayo  serikali inatarajia kuanza kuzalisha megawatts 30 za umeme wa jotoardhi ambapo mradi wa Kinyerezi umekamilika kwa asilimia 100, na kwamba hadi sasa imeingiza megawatts 218 kwenye grid ya taifa na kufikia mwisho wa mwezi Septemba  megawatts zote zitakuwa zimeingia.

*Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO*

 

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa