MGANGA Mkuu wa Manispaa ya Songea Dk.Mameritha Basike anawatangazia wananchi wote wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika wiki hii ya kuchangia damu kwa hiari katika vituo vya Manispaa ya Songea kikiwemo Kituo cha Afya Mjimwema na kituo cha soko kuu la mjini Songea ili kuchangia damu kwa hiari.Unashauri kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wengine.Kulingana na Dk.Basike kila kituo kimepangwa kukusanya damu uniti 100 ambapo katika kituo cha soko kuu na Kituo cha Afya mjimwema lengo ni kukusanya uniti 200 ambazo zitasaidia kupunguza mahitaji ya damu kwenye vituo vya afya na hospitali.JITOE KWA AJILI YA MWINGINE,CHANGIA DAMU.WOTE MNAKARIBISHWA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa