CHANJO ya kutokomeza magonjwa ya surua,rubella na polio inatarajia kufanyika katika Manispaa ya Songea kuanzia Oktoba 17 hadi 21 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyowashirikisha wataalam na viongozi wa dini,mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema,chanjo hiyo ni muhimu kufanyika kutokana na takwimu kuonesha kuwa ni kati ya asilimia 85 ya watoto wanaopata chanjo ya surua hupata kinga kamili.
“Kuna mlundikano wa watoto wasiokuwa na kinga katika kila mwaka ambao wanaweza kusababisha mlipuko wa surua’’,amesema Mgema.
Hata hivyo Mgema amesema kampeni ikisimamiwa vema na uhamasishaji wa kutosha hasa katika ngazi ya jamii,watoto wengi wanaweza kufikiwa na huduma ya chanjo hivyo kuwafikia watoto wasiochanjwa kabisa na kuwaongezea wale waliopata.
Kwa upande wake Mratibu wa chanjo katika Manispaa ya Songea Wilibert Mhalule amesema chanjo ya polio ilianza kutolewa hapa nchini Aprili 2018 na kwamba lengo lilikuwa ni kuanzisha chanjo hiyo tangu Aprili 2016.
Hata hivyo amesema uchunguzi umebaini kuwa hapa nchini kuna kundi kubwa la watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ambao hawajapata chanjo.
“Manispaa ya Songea inakadiriwa kuwa na watoto 36,312 chini ya miaka mitano,lakini walengwa wa kampeni hii ni 25,542 kwa chanjo ya surua rubella ni watoto 17,018 ndiyo wanaotarajiwa kupata chanjo ya polio ya sindano.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa