• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

CHIWINDI;Mto unaoongoza kwa uchafuzi ziwa Nyasa

Tarehe ya kuwekwa: October 22nd, 2018

MKUU wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma  amekagua Msitu wa Hifadhi ya asili ya Chiwindi yenye ukubwa wa hekta 3000 iliyopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

 Uchunguzi umebaini kuwa kuna uchafuzi wa kutisha katika Mto Chiwindi unaopita ndani ya hifadhi hiyo.Mto huo ambao unatumiwa na nchi zote mbili upo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

 Mto huo unamwaga maji yake ziwa Nyasa ni mchafu mwaka mzima kutokana na kuchafuliwa na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu toka nchi zote mbili ambao wanatumia kemikali ya zebaki kusafishia dhahabu.

 Uchunguzi uliofanya na Bonde la Maji la ziwa Nyasa unaonesha kuwa kati ya mito mikubwa minane inayoingiza maji katika ziwa Nyasa,mto Chiwindi unaoongoza kwa uchafuzi wa taka za zenye sumu ambazo zinaleta athari kubwa kwa viumbehai wa mtoni na ziwa Nyasa.

 Mkuu wa wilaya  na ujumbe wake walivuka mpaka wa Tanzania na kuingia nchini Msumbiji katika wilaya ya Kobwe Jimbo la Niassa na kuzungumza na wananchi hao juu ya umuhimu wa kuwaelimisha wananchi wa pande zote mbili kuacha kutumia kemikali zenye sumu katika mto Chiwindi na kuhifadhi msitu wa Chiwindi ambao nchini Msumbiji unaitwa Shiwindi.

 Chilumba amewaeleza wananchi wa Msumbiji kuwa Agosti mwaka huu ulifanyika mkutano wa ujirani mwema baina ya Tanzania na Msumbiji katika hoteli ya Hunt Club ya Songea mkoani Ruvuma.

 Mkutano huo ulishirikisha watendaji na wakuu wa wilaya za mikoa ya Mtwara na Ruvuma na wakuu wa wilaya na magavana wa majimbo ya  CaboDelgado na Niassa toka nchini Msumbiji.Mkutano huo pia uliwashirikisha balozi wa Msumbiji nchini Tanzania na balozi wa Tanzania nchini Msumbiji.

 Mkutano ulipitisha maazimio 12 ambayo yanahitaji utekelezaji ambao utatoa matokeo makubwa.Moja ya maazimio hayo ni kuongeza jitihada za kulinda mazingira katika Bonde la ziwa Nyasa nchini Tanzania na Bonde la Niassa nchini Msumbiji kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa