Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtella Mwampamba amewataka wazazi kutoa ushirikiano kwa walimu, pamoja na watendaji na kuendelea kuchangia chakula kwa wanafunzi shuleni ili watoto waweze kuwa na Lishe bora na utulivu wakati wa masomo.
Kauli hiyo imetolewa katika kikao cha utekelezaji wa mkataba wa lishe kilichofanyika tarehe 15 August 2024 katika ukumbi wa TTCL Manispaa ya Songea ambacho kilihudhuriwa na Watendaji wa kata 21 za Manispaa ya Songea kwa lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ngazi ya Kata katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2024.
Mtella alisema “ ni lazima tuwaambie wazazi umuhimu wa kutoa mchango wa chakula shuleni ambacho kitamsaidia mwanafunzi kupata chakula kwa pamoja awapo mazingira ya shule na endapo mzazi hatachangia chakula cha mtoto wake hiyo haipelekei kumkomoa mwalimu au Afisa Mtendaji bali inamjengea mazingira magumu mtoto wake mwenyewe” Alisisitiza.
Aliongeza kuwa huwezi kujitegemea kama utaishi bila umoja, uwezi kujitegemea endapo huna uzalendo hivyo amewataka wazazi/walezi kuondoa ubinafsi na kuwajenga tabia ya umoja watoto wao ili waweze kuwa kizazi chenye uzalendo hapo baadae.
Aidha, alimpongeza Afisa Mtendaji wa Kata ya Lilambo Teah Komba kwa kufanya vizuri katika kusimamia utekelezaji wa afua za lishe ngazi ya Kata ambapo katika kipindi cha mwaka 2023/2024 kata ya lilambo imeongoza na kuwa ya kwanza kwa kupata asilimia 96.79. Alipongeazwa.
Kwa upande wake afisa Lishe Manispaa ya Songea Albert Sinkamba alisema katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2024, kiashiria cha wanafunzi wanaokula chakula chenye viini lishe shuleni ni asilimia 10.4 ambacho bado elimu inaendelea kutolewa ili kufikia asilimia kubwa ambapo wataongeza usimamiaji kwa wazabuni wote wanaopeleka chakula shuleni wahakikishe wanaweka viini lishe.
Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Lilambo Teah Komba ameishukuru Serikali kwa kuanzisha Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ngazi ya kata na Mitaa ambvayo inawezesha jamii kuondokana na udumavu na utapiamlo kwa watoto chini ya miaka 5, pia ameshukuru uongozi wa kata, na mitaa na kwa kushirikiana na wananchi wameweza kuongoza kuwa wa kwanza katika afua ya lishe ngazi ya kata.
IMAEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa