DIRA ni muongozo unaotumika kuonesha nini cha kufanya, eneo la kufanya, na wakati wa kufanya na watu wa kuwafanyia ambayo inaweza kuwa ya muda mfupi wa miaka 5, au muda mrefu wa miaka 25,50 au 75.
Kutokana na umuhimu wa kuwa na maendeleo yanayotokana na Falsafa thabiti, inayoongozwa na wananchi wenyewe ndipo wazo la DIRA ya maendeleo ya muda mrefu lilipojitokeza ambalo ni azma ya Serikali ya kuamsha matumaini na uzalendo wa wananchi ndipo Serikali ilipokuja na DIRA ya kwanza ya Maendeleo ya Taifa.
Hayo yamejiri wakati wa kikao cha awali cha maandalizi kuhusu DIRA ya Taifa ya Maendeleo 20250 ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambacho kilihudhuriwa na wadau mbalimbali, Viongozi wa dini, vyama vya siasa, na wataalamu kutoka katika Halmashauri za Wilaya ya Songea kwa lengo la kutoa maoni ya DIRA ya Taifa ya Maendeleo ya 2050
Akizungumza Katibu Tawala Wilaya ya Sopngea, Ndugu Mtella Mwampamba ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Songea, ambapo alisema” Mwaka 2000 chini ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjamini William Mkapa (R.I.P) ambaye ndiye Mhasisi wa DIRA alikuja na DIRA ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 ambayo inaendelea kutekelezwa hadi sasa.”
Mwampamba alibainisha kuwa, DIRA ya maendeleo ya mwaka 2025 imewzesha kuleta mafanikio ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ikiwemo na Nchi kuingia kwenye nchi za kipato cha kati,na kuimarika kwa huduma za Elimu kwa ngazi zote (Kitaifa, kikanda, Kimkoa, Kta na ngazi ya kata.)
Aidha, Kufuatia ukomo wa utekelezaji wa DIRA ya 2025, Serikali kupitia Tume ya Mipango imeshaanza mchakato wa maandalizi ya Dira mpya ambao ulizinduliwa rasmi na Mheshimiwa Dkt. Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwezi Aprili mwaka 2023 Jijini Dodoma.
Kwa upande wa Washiriki wa Kikao hicho walipongeza Serikali kwa kuwa DIRA ya Taifa ya Maendeleo ambayo ni muongozo unaotumika katika kuonesha nini cha kufanya, eneo la kufaya, wakati wa kufanya na kuifanyia jamii.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa