MKUU wa Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma, Isabela Chilumba amemzawadia bango linalozunguzia kilio cha mti mtoto mmoja baada ya kuhudhuria mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mtupale kata ya Chiwanda wikayani Nyasa.Mkutano huo ambao ulilenga kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi wa kijiji hicho kilichopo mpakani mwa Tanzania na nchi ya Msumbiji.Mkuu huyo wa wilaya alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kukagua msitu wa asili wa Chiwindi ambao upo katika kijiji hicho,pia kufanya mkutano wa hadhara kwa lengo la kutoa elimu ya Uhifadhi toka kwa watalaam wa Maliasili ngazi ya wilaya na mkoa.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa