Mkuu wa wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile amewataka Maafisa wa Watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha wanasimamia zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya mitaa wanayoongoza.
Agizo hilo limejiri wakati wa kikao kazi cha Mkuu wa Wilaya ya Songea chenye dhamira ya kujitambulisha kwa watumishi wa Manispaa ya Songea kilichofanyika leo tarehe 02 Februari katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mhe.Ndile ameanza kwa kutoa shukrani kwa Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kumteua na kumwamini kumpa nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Songea ambapo amewataka watumishi hao kutoa ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya Serikali ili kufanikisha lengo lililokusudiwa.
Aliongeza kuwa Duniani kote kuna watumishi wamewekwa kwa lengo kuu ni kurahisisha namna ya utendaji wa kazi pamoja na kutekeleza wajibu wa Serikali uliowekwa wa kutoa huduma bora kwa jamii bila vikwazo vyovyote. “ Mhe. Ndile alisisitiza.”
Amebainisha kuwa “ Katika utumishi wa umma mahusiano na ushirikiano ni jambo jema sana ambalo huwezesha mtumishi kupata amani na furaha katika mazingira ya kufanyia kazi ambayo husaidia kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu ya Serikali. Alisisitiza”
Amewataka watendaji wa Kata na Mitaa pamoja na Idara ya Elimu kuhakikisha wanafuatilia suala la wanafunzi wasioripoti shule wa kidato cha kwanza ambapo amewataka wazazi wote ambao watoto wao hawajawapeleka shule wahakikishe wanawapeleka watoto wao kabla hawajachuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewataka watumishi kuwajibika kufanya kazi kwa kila mtu katika eneo lake na msifanye kazi kwa mazowea na kuhaidi kuwa maagizo na maelekezo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi.
Mwisho.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa