• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DC SONGEA ATOA AGIZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA KUSIMAMIA MKATABA WA LISHE KIKAMILIFU.

Tarehe ya kuwekwa: April 16th, 2021

Mikoa ya nyanda za juu kusini,  utafitI unaonyesha ndiyo inayoongoza kuwa na kiwango kikubwa cha watoto wenye udumavu na utapiamlo.

Kauli hiyo imebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akiwa katika kikao cha tathimini ya Lishe Manispaa ya Songea kilichohudhuriwa na maafisa wa Watendaji Kata 21 na wataalamu wa afya kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea jana tarehe 15 aprili 2021.

Pololet alisema lengo la kuweka tathimini katika kila robo moja ya mwaka  ni kuweka mkakati na mpango kazi wa lishe bora kwa jamii  ili kuhakikisha tunapunguza au kuondoa kabisa tatizo la watoto wenye udumavu na utapiamlo Mkoani   Ruvuma hasa Songea Mjini.

Aliongeza kuwa  nyenzo muhimu ya kutekeleza mkakati wa lishe Manispaa ya Songea ni kutoa elimu kwa jamii ili kuondoa changamoto zinazojitokeza za ongezeko la watoto wenye udumavu na utapiamlo kwa watoto walio chini ya miaka mitano 5  kutoka asilimia  0.08%  septemba 2020 hadi asilimia 0.16%   januari hadi machi ikiwa ni ongezeko kubwa kuliko kipindi cha nyuma.

Alisema ongezeko hilo linatokana baadhi ya akimama wajawazito kutohudhuria kliniki kwa wakati, wahudumu wa afya na watendaji wa kata na Mitaa  kutotembelea kaya zenye wajawazito na watoto walio chini ya miaka mitano 5,  ukosefu wa elimu  ya Lishe kwa Maafisa watendaji wa kata na Mitaa, pamoja na kukosekana kwa sheria ndogo ndogo za mkataba wa lishe kwa watoto walio chini ya miaka mitano 5.

Pololet amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Songea Tina Sekambo kuwawezesha Maafisa wa watendaji wa kata kupata elimu ya mafunzo ya Lishe ili waweze kutoa elimu sahihi ya lishe kwa jamii, pamoja na uandaaji wa taarifa zenye takwimu sahihi, uwajibikaji wa kazi na uwazi wa utawala bora katika maeneo yao ya kazi  kwa  kubandika taarifa za kiutendaji katika mbao za matangazo pamoja na kuzingatia kanuni ya  uendeshaji wa vikao vya kisheria ifikapo kila robo moja ya mwaka na uandaaji wa sheria ndogo za lishe.” Alisisitiza” .

Naye Afisa Lishe Manispaa ya Songea Florentine Joseph Kissaka alisema jumla ya watoto wenye utapiamlo mkali waliopewa rufaa kwenda kwenye matibabu ni 29 ambao  walitoka kata za matarawe 1, misufini 1, matogoro 21, Ruhuwiko 1, na Msamala 5 kati ya watoto 17,840 waliopimwa sawa na asilimia 0.16  ya wenye utapiamlo katika kipindi cha januari-machi.

Kissaka alibainisha kuwa jumla ya vijiji vilivyofanya mkutano siku ya afya na lishe ni 91 kati vijiji 95 sawa na asilimia 95.8% ya  utekelezaji wa zoezi hilo. Aliongeza kuwa vijiji vyenye sheria ndogo za lishe ni 77 kati ya vijiji 95 sawa na asilimia 81.1%,  vijiji vilivyobandika taarifa ni 86 kati ya vijiji 95 sawa na 90.5%.

Miongoni mwa mikakati iliyowekwa ili kukabiliana na ongezeko la watoto wenye udumavu na utapiamlo Manispaa ya Songea ni pamoja na kuendelea  kutoa elimu  kwa jamii namna ya uandaaji wa chakula cha  lishe kwa mtoto chini ya miaka mitano, mpangilio wa ulaji wa chakula, na aina ya chakula kinachofaa kuliwa.

 IMEANDALIWA NA;

AMINA PILLY;

AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.

16 APRILI 2021

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa