Duniani kote hakuna Serikali inayoendeshwa bila kodi. Bila kukusanya kodi na tozo mbalimbali zilizowekwa kwa mujibu wa sheria, hatuwezi kufanikiwa.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema akiwa katika kikao kazi na Maafisa watendaji wa Kata, Maafisa watendaji wa mitaa, Wakuu wa idara pamoja na wataalamu kutoka TRA kwa ajili ya kuhimiza ukusanyaji wa kodi za majengo kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea 10/02/ 2021.
Pololet alisema kwa kipindi cha miaka ya nyuma kodi za majengo zilikuwa zikikusanywa na Serikali za mitaa wakati huo Halmashauri zilikuwa zikitegemea kuwa chanzo chake cha mapato ya ndani lakini miaka ya hivi karibuni baada ya Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani kodi kodi hiyo ya majengo ilihamishiwa TRA.
Aliongeza kuwa kutokana na ukubwa wa kazi hiyo na uchache wa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato TRA, Serikali imeona ni vyema kazi hiyo irudishwe kwenye Halmashauri zote Nchini ili kuongeza ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa kazi hiyo.
Pololet alibainisha kuwa, kwa kushirikiana na Watendaji wa kata na mitaa anaamini kuwa kazi hizo zitafanyika kwa ufanisi mkubwa kutokana na uzoezi wa awali wa kusimamia kukusanya mapato yatokanayo na kodi za majengo. Alisema, wataanza na zoezi la uhakiki wa majengo yote yenye sifa za kulipia kodi za majengo ili kupata kazi data (takwimu) halisi ambazo zitasaidia kuleta ufanisi katika ukusanyaji wa kodi za majengo pia mapato hayo ya takusanywa kwa kutumia mfumo wa kieletroniki.
Ili tuweze kuboresha huduma mbalimbali za kijamii nilazima kukusanya kodi ambayo inasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo kwa jamii, nanukuu “ Mwl Nyerere alisema Nchi ambayo haikusanyi kodi haiwezi kujiendesha. Ili iweze kujiendesha nilazima ikusanye kodi” mwisho wa kunukuu.
Akizitaja faida za ukusanyaji wa kodi hizo ambapo alisema hadi kufikia mwaka 2015 tulikuwa na Hosptali za Wilaya 66 tu, pia kufikia mwaka 2020 kuna ongezeko la Hospitali za Wilaya 102, vituo vya afya 487 pamoja na miradi mingine mingi mikubwa inayoendelea kutekelezwa.
Naye Afisa kodi msaidizi Batilda Simon kutoka TRA alisema sheria inayotuongoza katika ukusanyaji wa kodi za majengo mamlaka za Miji ya mwaka 1983 na sheria ya fedha 2016/2017 na sheria ya mwaka 2017/2018 pamoja na kanuni za ukusanyaji wa kodi za majengo iliyotangazwa katika gazeti la Serikali 03 januari 2020 ambayo imeainisha mambo muhimu ambayo wakusanyaji nilazima wayafuate.
Batilda alisema sheria hizo zimeainishwa pamoja na wajibu wa mmiliki wa jengo, viwango vya ulipaji, wajibu wa Serikali za mitaa, njia za ulipaji, na msamaha wa kodi za majengo ambapo alieleza bayana kuwa msamaha wa kodi za majengo utatolewa kwa mmiliki mlemavu/ mwenye umri wa miaka 60 au Zaidi lakini nyumba hiyo isiwe imepangishwa pia msamaha huo utatolewa kwa kuhuwisha taarifa zake kila mwaka wa fedha yaani tarehe 01 julai.
Alisema endapo mmiliki atakataa kulipa /kushindwa kutekeleza maagizo hayo/ kukataa kutoa taarifa zake atatakiwa kulipa adhabu ya kiasi cha shilingi 100,000/= laki moja au kulipa mara nne ya kiasi anachodaiwa ama kifungo cha mwezi mmoja 1 lakini kisizidi miezi mitatu 3.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
11 FEB 2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa