Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ametembelea mradi wa Machinjio ya kisasa iliyopo kata ya Tanga Manispaa ya Songea na kuzindua jaribio la awali la matumizi ya mashine mpya na ya kisasa ya kuchinjia nyama liililofanyika leo tarehe 22 Januari 2021.
Pololet alisema machinjio hii kwa ukubwa wake imegharimu billion 5.7 ambao endapo kama wateja watapatikana inakadiliwa kuchinjwa ng’ombe kati ya 100 hadi 200 kwa siku moja pia inasaidia kuonyesha uzito wa ng’ombe aliyechinjwa, muda aliochinjwa, ubora wa nyama yenyewe, pamoja risiti/ billi ya iliyo lipwa.
Amewataka wataalamu hao kutafuta masoko nje ya Mkoa/ Nchi ili kutangaza biashara kwa kuwapata wawekezaji wengi Zaidi ili machinjio iweze kufanya kazi kwa ufanisi na kutimiza malengo tarajiwa yaliyowekwa na serikali.
Ametoa rai kwa wachinjaji hao kufanya kazi kwa ufanisi ikiwemo na kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji ili waweze kufanikisha kuchinja ng’ombe mmoja kwa kwa haraka na kwa kutumia dakika 10 hadi 15 na hatimaye waweze kuhudumia sehemu kubwa Zaidi.
Alisema baada ya kukamilika kwa asilimia 100% za maandalizi ya maeneo machinjio hayo itatakiwa kufunga machinjio ya Msamala na maeneo mengine yote yanayochinja nyama kwa lengo la kuhakikisha nyama zote zinazoliwa zinakuwa safi, salama kwa walaji.
Akizitaja faida zitakazopatikana baada ya kufunguliwa kwa machinjio hiyo ni pamoja na ongezeko la ajira, kuongezeka kwa mapato, pamoja na upatikanaji wa nyama bora.
Machinjio hiyo inatarajiwa kuanza kazi hivi karibuni mara baada ya kukamilika kwa maandalizi mbalimbali ya kiutendaji.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
22.01.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa