DC SONGEA, AKAGUA UJENZI DARAJA LA MATARAWE
MKUU wa Wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma Palolet Kamando Mgema leo amefanya ziara ya kushitukiza kukagua ujenzi wa daraja la Matarawe lililopo katika Manispaa ya Songea.Daraja hilo ni kiungo muhimu cha wananchi wa Kata za Matarawe, Mjimwema na kata nyingine jirani.Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Eng. Samwel Sanya amesema zaidi ya sh.milioni 127 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.Mradi huo ni wa miezi sita,ulianza Juni 2017 na unatarajia kukamilika Desemba 2017.
Ubovu wa daraja hilo umekuwa kero kwa wananchi wa Manispaa ya Songea hali ambayo imesababisha ajali za mara kwa mara.Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea kumsimamia Mkandarasi ili aongeze kasi ya ujenzi wa daraja hilo ili mradi uweze kukamilika kwa haraka na wananchi waanze kulitumia daraja ambalo ni kiungo muhimu kwa mawasiliano ya barabara.
Licha ya kukagua daraja hilo,Mkuu wa Wilaya ya Songea pia ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi katika Manispaa ya Songea na kutoa maagizo ya kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo kwa wakati.
Taarifa imetolewa na
Albano Midelo,Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa