Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro (MB) amewataka wananchi wa Manispaa ya Songea Kutumia fursa ya Msaada wa kisheria Mama Samia inayoendelea kutolewa katika wiki ya Msaada wa Kisheria iliyozinduliwa kitaifa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.
Hayo yamejiri katika Ziara ya Mhe. Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini iliyofanyika tarehe 25 julai 2023 akiwa katika Kata ya Matogoro iliyofanyika kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za Wananchi.
Akizungumza na Wananchi, Dkt. Ndumbaro (MB) alisema “ Tarehe 17 Julai alitembelea kata ya Matogoro kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi ambapo Wananchi waliwasilisha Changamoto zao ikiwemo na Ombi la kompyuta, na Saruji ambapo alitoa Msaada wa Saruji mifuko 10, Kompyuta moja 1 pamoja na fedha shilingi 1,000,000 kwa ajili ya matengenezo ya kisima cha shule.”
Dkt. Ndumbaro alisema Shule ya Msingi Matogoro imepokea fedha Mil. 40 kwa ajili ya ukarabati wa wa madarasa yote chakavu ambapo utelezaji wa mradi huo unatarajia kuanza mwaka Mpya wa fedha 2023/2024.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara iliyoanza kufanyika tarehe 17 julai 2023 ambapo alifanikiwa kutembelea kata ya Matogoro, Kata ya Bombambili, Kata ya Mletele, Kata ya Mshangano, Kata ya Tanga, pamoja na kata ya Ruhuwiko.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa