AFISA UCHAGUZI Manispaa ya Songea Buruhani Mapunda amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na maelekezo yote ya Uchaguzi yatakayotolewa na Mamlaka ya Uchaguzi ambayo ni Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Elimu hiyo inaendelea kutolewa kwa nyakati tofauti kupitia mikutano ya hadhara ya wananchi na kongamano kwa wanafunzi wa shule za Sekondari kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi na jamii kuanzia miaka 18 kuishiriki kujiandikisha, kuchagua na kuchaguliwa.
Alisema Mwananchi anawajibu wa kushiriki kwenye mikutano ya kampeni kwa lengo la kufahamu uwezo wa kiongozi anayefaa, kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi, kuhamasisha jamii kujiandikisha na kuchagua kiongozi, kushirikiana na viongozi baada ya uchaguzi katika kuleta maendeleo, pamoja na kupinga Rushwa kwa lengo kuihamasisha jamii juu ya uwepo wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu 2024.
KAULI MBIU ya mwaka 2024 ni “Uhifadhi wa Mazingira na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa