Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba amewataka wananchi wa Kata ya MwengeMshindo kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi la Uhakiki wa majina ya wadai Fidia (EPZA) ya viwanja/nyumba/mashamba ili kuondoa malalamiko yanayoweza kuathiri utendaji wa zoezi hilo.
Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea alisema “EPZA wamekuja kulipa fidia ya viwanja na kila mwananchi mnufaika wa fidia hizi atalipwa kulingana na ukubwa wa eneo lake, na kila mnufaika atalipwa fidia kulingana na uthamini uliofanyika bila udanganyifu wowote.” Alisistiza”
Hayo yamejiri wakati wa Mkutano wa wananchi wa Kata ya Mwengemshindo uliofanyika tarehe 02 Agost 2023 uliohudhuriwa na viongozi ngazi ya Wilaya, Halmashauri, EPZA pamoja na wananchi kwa lengo la kufanya uhakiki wa wananchi wanufaika watakaolipwa fidia ya ardhi kata ya Mwengemshindo.
Mwampamba aliwapongeza wananchi wa Kata ya Mwengemshindo kwa kuwa na uvumilivu na upole wakati walipokuwa wanasubili Serikali ianze mchakato wa kulipa madai ya wananchi 900 kwa Hekta za mraba 5000.
Aliwapongeza Viongozi wa Serikali ikiwemo na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Ardhi, Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Viongozi ngazi ya Mkoa na Wilaya, Halmashauri, pamoja na Mhe. Diwani wa Kata ya Mwengemshindo kwa ufuatiliaji wa mara kwa mara na kufanikiwa kulipa fidia hizo ambazo zitaondoa kero kubwa kwa wananchi wa kata hiyo. Alibainisha.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa EPZA Charls Itembe alisema” nianze kwa kuwapongeza viongozi ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya na ngazi kata wamefanya kazi kubwa sana ya kushawishi, kufuatilia madai haya ambayo yamefikia hatua ya ukamilishaji wa malipo ya fidia kwa wananchi wa mwengemshindo. “Alipongeza”
Itembe alisema malipo hayo kwa mara ya kwanza yalilipwa kwa baadhi ya wananchi na awamu ya pili yatatolewa kwa ambao hawakulipwa ambapo kabla ya kuanza kulipwa yataanza na uhakiki wa majina yao utaofanyika kwa muda siku nne 4 katika ofisi ya kata Mwengemshindo ambapo watahakikiwa kwa kuleta viambatanisho ikiwemo na kitambulisho, picha, pamoja na barua kutoka Serikali ya Mitaa ili malipo yalipwe kwa mtu anayestahili pia malipo yote yatalipwa kwa kupitia Akaunti za Benki.
Amewataka viongozi wa Serikali ya Mtaa kuhakikisha wanasimamia na kuhamasisha wananchi waweze kujitokeza ili kusiwe na malalamiko na baada ya kuhakikiwa kwa utaratibu wa kisheria jedwali hilo litatakiwa likahakikiwe ili kuanza malipo ya fidia.
Serikali ya awamu ya sita imejikita zaidi na dhana ya uwekezaji katika uwekezaji kiuchumi na baada ya kukamilisha malipo hayo eneo hilo litatakiwa kuwa na hati miliki ili kuweka fursa ambazo zitaongeza thamani ya uchumi.
Kwa upande wake Mthamini wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Alex Mshana alibainisha kuwa “kero kubwa ya wananchi wa Mwengemshindo ilikuwa ni madai ya fidia ambayo mara baada ya malipo ya fidia wananchi watatakiwa kupisha maeneo yaendelezwe na uwekezaji wa matumizi ya umma.
Naye Diwani wa Kata ya Mwengemshindo Oswin Kapinga ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kufanikiwa kulipa Fidia kwa wananchi wa kata ya Mwengemshindo, fidia inyolingana na mwaka wa fedha husika.
Kwa upande wa Wananchi wa Kata ya Mwenge Mshindo walitoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kulipa fidia kwa wananchi ambazo ilikuwa kero kubwa kwa wakazi wa kata hiyo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa