Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano ametoa wito kwa wafugaji wa ng’ombe, mbuzi, punda, na kondoo kupeleka mifugo yao kwenye maeneo pangiwa kupitia kila kata husika kwa ajili ya kufanya utambuzi, usajili,na ufuatiliaji wa wanyama kwa lengo la kuvika Heleni za kieletroniki ( Electronic eartags) ambayo itawezesha kutambulika mahala ilipo na umiliki wake.
Utekelezaji wa zoezi hilo umezingatia sheria ya utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo ya mwaka 2010 na kanuni zake 2011, Sera ya Taifa ya maendeleo ya mifugo ya mwaka 2006 na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025.
Hayo yamejili katika uzinduzi wa uvikaji wa heleni kwa mifugo iliyozinduliwa tarehe 20 Oktoba katika Mtaa wa Likuyufusi kata ya Lilambo iliyoshirikisha wafugji wa ng’ombe, mbuzi, punda ambapo zoezi hilo litahitimishwa tarehe 31 Oktoba 2022 kwa lengo la kupata takwimu na kukabili magonjwa ya mlipuko, usalama wa chakula kwa walaji, kurahisisha biashara ya mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi, udhibiti wa mifugo, kurahisisha upatikanaji wa mifugo iliyopotea na upatikanaji wa mikopo.
Mhe. Mbano amesema kuwa endapo mfugaji atahitaji kuuza au kununua mifugo atatakiwa kuwajibika kutoa taarifa kwa afisa mifugo wa mtaa au kata husika kwa mifugo yoyote itakayotolewa zawadi au itakayotolewa mahari ili kubadilishwa umiliki wake.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Lilambo Yobo Mapunda alieleza kuwa kata ya Lilambo ina jumla ya Ng’ombe 3028 hivyo amewataka wananchi wenye mifugo wote kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kufanya utambuzi na usajili wa mifugo yao kwa lengo la kudhibiti upotevu wa mifugo.
Naye Dkt. Seria Shonyela amesema utambuzi wa mifugo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea unafanyika katika kata 21, kwa idadi inayotarajia kutambuliwa kwa kuvikwa hereni ni ng’ombe 5,405, mbuzi 4,992, kondoo 125, na punda 151 ambao watawekwa alama maalumu ya keletroniki (BARCODE) ambayo itaweza kusomwa kwa kutumia kifaa maalum ambapo kila mfugo utagharimu kiasi cha shilingi 1,750 kwa kila ng’ombe, na shilingi 1000 kwa mbuzi na kondoo.
Kwa upande wa wafugaji walioshiriki katika zoezi hilo walisema “ wanaipongeza Serikali kwa kuanzisha zoezi la utambuzi wa mifugo ambayo itasaidia udhibiti wa upotevu wa mifugo yao.”
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa