Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Workers compensation Fund dependant compensation claims form ( ni Taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoundwa kwa mujibu sheria ya fidia kwa wafanyakazi yenye lengo kuu la kuanzishwa kwa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi ni kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi waliopo katika Sekta Rasmi (Umma na Binafsi) Tanzania Bara ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.
Afisa Madai Mwandamizi Ibrahim Iyombe kutoka ofisi ya Mfuko wa jamii (CWF) Dar es salaam akitoa mafunzo elekezi kwa watumishi wa manispaa ya Songea, yaliyofanyika 31.12.2020 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Iyombe alibainisha kuwa WCF ni mfuko wa Serikali ambao husaidia kulipa fidia kwa mtumishi kwa wakati kwa watu walioumia kutokana na kazi, kuugua, kufariki huku akitekeleza jukumu lake la kazi pamoja na jukumu la kuzuia au kukinga ajali na vifo kazini kwa kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi wenyewe.
Alisema“ mfuko huo hutoa huduma Kama kuna tukio la ajali, ugonjwa au kifo wakati Mfanyakazi akitekeleza majukumu yake ya ajira Mfanyakazi akiwa ameumia au ameugua au kufariki kutokana na tukio la ajali au ugonjwa utokanao na kazi, au Mfanyakazi amepata ulemavu.
Aliongeza kuwa WCF hutoa huduma za matibabu, malipo ya ulemavu wa muda, malipo ya ulemavu wa kudumu, malipo kwa anaye hudumia mgonjwa, huduma za ukarabati na ushaurina nasaha, malipo kwa tegemezi endapo mwanachama amefariki, na malipo ya msaada wa mazishi / rambirambi, huduma za kumsafirisha mgonjwa.
Mfanyakazi atapata malipo haya endapo atapata majeraha yanayotokana na ajali kazini au ataugua kutokanna kazi na kumfanya apate ulemavu wa muda mfupi. Malipo haya yatatolewa kwa kipindi kisichozidi miezi 24. Alisisitiza Iyombe.
Fidia ya malipo ya ulemavu wa muda utategemeana na ukubwa wa jeraha au ugonjwa na muda utakaokadiriwa na daktari, Kwa ulemavu wa muda mfanyakazi atapata fidia ya 70% ya kipato cha mwezi cha mfanyakazi wakati wa ajali au ugonjwa, kutegemea na muda na asilimia ya ulemavu.
Aliongeza kuwa Kama tukio la ajali/ugonjwa/kifo limetokea, au tukio hilo limepelekea kuumia/ugonjwa/kifo pia Mwajiri anatakiwa kutoa taarifa ofisi kuu Mfuko wa jamii ndani ya siku 7 kwa kutumia Fomu WCN- 1 ikiambatana na ripoti ya vipimo kutoka hospitalini inayoonyesha kugundulika kwa ugonjwa (Medical Diagnosis report,)
Aidha Baada ya kupokea taarifa ya ugonjwa Mfuko utafanya tathmini ya awali ili kuthibitisha kama ugonjwa huo unatokana na kazi au laa.
Kama ugonjwa utagundulika umetokana na kazi, Mfuko utamruhusu mwajiriwa kupata matibabu chini ya Mfuko na taratibu za fidia kuendelea.
Aidha, watumishi waliohudhuria mafunzo hayo wamepata kufahamu elimu namna ya kujisajili, kuwasilisha michango yao WCF, na namna ya kudai fidia pamoja na mafao yote yanayotolewa na mfuko wa WCF.
Mwisho alisema mfuko huo hauhusiki katika kutoa huduma kwa mtumishi za magonjwa sugu kama kansa labda chanzo cha ugonjwa huo uwe unasababisha na mazingira ya kazini au ajali kazini.
IMENDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
31 Ddisemba 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa