Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania, imefanya maadhimisho ya siku ya ufugaji nyuki duniani ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 20 Mei ya kila mwaka, ambapo kutokana na kuwepo kwa janga la corona duniani, mwaka huu maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa hapo jana tarehe 29 Julai 2021 katika uwanja wa Majimaji Mjini Songea Mkoani Ruvuma.
Katika kutekeleza mkakati wa sera ya Taifa ya ufugaji nyuki ya mwaka 1998 yenye malengo 6 ambayo yatatekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2021 hadi 2031 ikiwemo na kutumia rasilimali misitu kwa ajili ya kuanzisha hifadhi za nyuki kwa lengo la kuongeza uchumi na pato la Taifa.
Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda ambaye alitoa elimu kwa wananchi na wataalamu mbalimbali kuhusiana na namna ya kufuga nyuki kibiashara ili kuongeza uchumi na pato la Taifa kiujumla pamoja na kuzindua vibanda vya wajasiliamali waliojitokeza kwenye maadhimisho hayo yaliyoambatana na uzinduzi wa tamasha la Majimaji Serebuka ambayo yalianza 24 julai na kumalizika 31 julai 2021.
Aliongeza kuwa kuna faida nyingi zitokanazo na zao la nyuki ambazo ni kuongeza virutubisho mwilini, pia sumu ya nyuki hutumika kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ikiwemo na kansa pamoja na Virusi vya Ukimwi (VVU). “Alibainisha”
Mizengo alihamasisha wananchi kutumia rasilimali misitu kama fursa kwa ajili ya kuanzisha hifadhi za nyuki ili kuwepo na upatikanaji wa mazao ya nyuki ya kutosha pamoja na kutengeneza ajira kwa vijana.’Alieleza’
Kwa upande wake Mbunge wa Songea Mjini na Waziri wa Maliasili na utalii Dkt. Damas Ndumbaro alimshukuru Mgeni rasmi kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusiana na ufugaji wa nyuki na ameahidi Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha zao la nyuki linakuwa bora barani Afrika na duniani kwa ujumla.
Kauli mbiu ya Maadhimishi ya siku ya ufugaji nyuki duniani ni;
“FUGA NYUKI KWA MAENDELEO YA VIWANDA NA USALAMA WA CHAKULA”
IMEANDALIWA NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
30.07.2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa