Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko amewataka kuchangamkia fursa za uwekezaji kuptia maeneo mbalimbali ya uwekezaji ambayo Halmashauri imetenga.
Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 07 Machi 2024 akiwa anazungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari Radio Jogoo na Selous FM, kwa lengo la kuwafahamisha wananchi juu ya uwepo wa Fursa za Uwekezaji zilizopo ambazo zitawezesha kuinua kipato cha mwananchi mmoja mmoja.
Dkt. Sagamiko alisema ili kufikia Jiji nilazima Songea ibadilike kwa kuwekeza kwenye maeneo ambayo tayari Serikali imeshawekeza miradi mikubwa kwa kununua viwanja kwa ajili ya uwekezaji wa Hotel, Vituo vya mafuta, Biashara pamoja na vituo vya mafuta.
Akibainisha maeneo ya uwekezaji ni pamoja na viwanja vilivyopo mbele ya Stand ya Tanga, Eneo la Nanenane Lilambo, Eneo la viwanda vidogo Lilambo, Subira, Mletele pamoja na Mwengemshindo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa