Serikali ya awamu ya sita imeweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa kahawa kutoka Tani 79,000 ambazo zimezalishwa sasa hadi kufikia Tani 500,000 ifikapo mwaka 2030 ambapo katika kufanikisha na kufikia malengo ni kushirikisha Halmashauri zote za Wilaya Nchini kupitia wakuu wa Wilaya.
Nchi imedhamiria na kujipanga kuimarisha maisha ya mkulima ambapo malengo ya Wizara ni kuhakikisha inakuza kilimo kwa 10% ifikapo 2030 ikiwa mchango wa kilimo katika Taifa letu ni 10% ambayo kwa kupitia mwenendo huo inawezekana.
Hayo yamejiri leo tarehe 06 Disemba 2023 katika mkutano wa kilimo cha kimkakati kwa zao la kilimo cha Kahawa Wilaya ya Songea uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambao umehudhuriwa Naibu wa Waziri wa kilimo, Viongozi ngazi ya Mkoa, Wilaya na Halmashauri pamoja na wananchi kwa lengo la kuweka mikakati na kufanya ufuatiliaji wa zao la Kahawa Wilayani humo.
Akizungumza Naibu waziri wa kilimo Mhe. David Silinde (MB) ambapo amesema “ Serikali imeweka utaratibu wa kugawa Ruzuku za pembejeo ambazo ziligawiwa kwa wakulima kuanzia mwaka 2022 na kuendelea kwa lengo la kuhakikisha wakulima wanapata uzalishaji wa kutosha kwa mazao yote Nchini.”
Mhe Silinde alisema Lengo la Serikli katika kusajili wakulima ni kupata takwimu sahihi za wakulima ambazo zitawezesha Serikali kujipanga kibajeti na kuhakikisha wakulima wanafanikiwa kupata Ruzuku za pembejeo. ‘Alibainisha.”
Aliongeza kuwa, lengo la Mhe Rais anataka kuona mkulima analima zaidi ya mara moja kwa mwaka na hataki kuona mkulima anategemea kilimo cha mvua bali anataka alime zaidi ya moja kwa mwaka kupitia kilimo cha umwagiliaji.
Kilimo cha zaidi ya mara moja kwa mwaka humsaidia mkulima kuongeza kipato chake binafsi ambacho itasaidia Serikali kuongeza pato la Taifa kwa mwaka ambapo hapo awali Bajeti ya kilimo ilikuwa chini ya Bilioni 960 na baada ya uongozi wa awamu ya sita kuingia madarakani bajeti imeongezeka mara nne zaidi kwa lengo la kuhakikisha inaleta katika kilimo.
Katika kufanikisha kilimo cha zao la kimkakati cha Kahawa amezitaka Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinatenga bajeti kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ili kuweza kupanda miche ya kisasa iweze kutoa ufanisi mkubwa.
Ametoa wito kwa maafisa kilimo wote kuhakikisha wanahamasisha, kuelimisha wakulima juu ya kupanda miche bora ya kahawa na kuachana na mitazamo ya kizamani ambayo haina tija kwa mkulima.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile, alisema Songea ina hali ya hewa nzuri,ina mvua ya kutosha, na ardhi bora yenye rutuba ambapo amewataka kulima kulima kilimo cha zao la kimakakti ambalo litasaidia kupata mapato ya kutosha.
Mhe. Ndile alisema zao la Kahawa linasaidia kupanda kwa uchumi ambapo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Songea inaingiza mapato ya ndani zaidi ya 45% licha ya kuwa na wakulima wachache wa zao hilo.
Wilaya ya Songea ndiyo yenye mashamba makubwa ya kahawa kupitia kahawa ya AVIV kuliko sehemu yoyote nchini au Afrika ya Kati ambapo pia kwa Manispaa ya Songea zao hilo hulimwa katika kata ya Ndilima litembo na Mahilo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa