Mheshimiwa Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea , amepongeza Maafisa Watendaji wa kata mbalimbali kwa kazi yao nzuri katika utekelezaji wa afua za lishe, akisisitiza umuhimu wa lishe bora kwa afya ya jamii.
Pia, ameagiza kuandikwa kwa barua za pongezi kwa Maafisa Watendaji, huku akiwataka kuwasilisha ripoti ya ulinganifu ya tathmini ya hali ya lishe ili kubaini changamoto na mafanikio.
Kwa upande wake Afisa Lishe Manispaa ya Songea Frolentine Kissaka, amesema kuwa miongoni mwa watoto 40,283 waliochunguzwa, asilimia 99.69 hawana utapiamlo, lakini watoto 19 waligundulika kuwa na utapiamlo mkali na kupatiwa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Hata hivyo hali hii inaonyesha hatua nzuri za Serikali katika kuhakikisha watoto na akina mama wanapata lishe bora, huku ikionyesha pia haja ya kuendelea na juhudi zaidi ili kuboresha hali ya lishe katika jamii.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea 01 Novemba 2024 ambacho kilihudhuriwa na Maafisa watendaji wa Kata, Viongozi ngazi ya Wilaya na Maafisa Lishe kilichofanyika kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa Mkataba wa Lishe ngazi ya Kata.
NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa