• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI ya Nyasa yaridhia ombi la uwekezaji toka Mwanza

Tarehe ya kuwekwa: September 16th, 2019

 Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa  Mkoani Ruvuma, imeridhia ombi la eneo la Uwekezaji  wa vizimba vya samak,i kutoka  Kampuni ya Mwanza Delights Compony ili kupunguza umaskini na kutokomeza uvuvi haramu Wilayani hapa .

akiwasilisha taarifa hiyo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani, cha Wilaya ya nyasa kilichofanyika hivi karibuni  katika Ukumbi wa Kepteni John komba Mjini Mbamba-bay,  Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa Bw.Jimson Mhagama aliwataka wajumbe kujadiliana kwa umakini na kutoa maoni yao.

Bw Mhagama alifafanua kuwa,  Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ilipokea ombi la eneo la uwekezaji pamoja na ujumbe wa watendaji wakuu kutoka kampuni ya mwanza Delights compony,  ikieleza lengo la kampuni hiyo kuja kuwekeza Nyasa, katika Ufugaji wa samaki kwa kutumia Vizimba, na maeneo yanayofaa kwa kilimo cha kakao,kahawa  na korosho.walipata uwepo wa maeneo hayo  kupitia maonesho ya viwanda na biashara yaliyofanyika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Aliongeza kuwa, baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya fukwe ambayo yaliainishwa na wataalam ujumbe kutoka mwanza Delights company ltd, uliridhishwa na eneo la fukwe ya puulu na kuona linafaa kwa ajili ya ufugaji kwa kutumia vizimba na maeneo ya Kijiji cha Lundo yanafaa kwa ajili ya Kilimo  cha mazao ya biashara yaani Korosho,kahawa na kakao.

Aidha aliongeza kuwa ,mradi wa vizimba utawajumuisha na kuwashirikisha na kuwawezesha wavuvi katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Nyasa ili kufuga samaki. Utaratibu huu utachangia kupunguza umaskini na tatizo la uvuvi haramu kwa kiwango cha kikubwa katika Halmashauri yetu. Pia mpango wa mradi wa kilimo utasaidia kuongeza fursa za ajira kwa jamii inayozunguka maeneo hayo, pamoja na kuongeza mapato ya ndani Katika Halmashauri ya Nyasa.

Baraza la madiwani kwa pamoja walikubaliana na taarifa hii na waliridhia kwa pamoja kupitia kwa Mwenyekiti wa Halmashauri Alto Komba  ambaye ni mwenyekiti wa kikao na kuwaomba wawekezaji wengine kuja kuwekeza nyasa kwa kuwa kuna sehemu nyingi  za uwekezaji.

“Napenda kuchukua Fursa hii kuwakaribisha sana wawekezaji katika Wilaya yetu ya nyasa kwa kuwa kuna Fursa nyingi za uwekezaji kwenye kilimo,ufugaji wa samaki wanyama,vivutio vya utalii vingi sana ambavyo viko nyasa” alisema komba.

Kampuni ya MDC  imejipanga kimkakati kutekeleza mradi huu kwani imeshakamilisha taratibu zingine zinazotakiwa katika utekelezaji wa Mradi ,hivyo waliomba kibali cha kutumia maeneo haya kwa ajili ya uwekezaji na utekelezaji wa miradi hii na wapo tayari kulipa fidia na wanaendelea na utafiti wa maeneo mengine hasa ya fukwe za njia ya kusini kwa Kata ya ( Kilosa,Mtipwili na Chiwanda)

Imeandaliwa na Netho c. Sichali

Kaimu Afisa Habari

Wilaya ya nyasa,0767417597

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa