DUNIA inakabiliwa na changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabianchi hali ambayo inaifanya Sayari ya Dunia kuwa njia panda.
Kutokana na hali hiyo viongozi wa nchi na serikali wa mataifa 150 duniani Desemba 2015 walifanya mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabia mjini Paris nchini Ufaransa,wakijitwisha dhamana ya mpango wa kihistoria wa kuepusha maafa ya ongezeko la Joto duniani.
Viongozi hao walipendekeza mpango wa kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaofanywa na binadamu na kuepusha athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabia nchi ambazo zinaweza kuangamiza viumbehai wote duniani.
Katika mkutano huo ulioshirikisha watu zaidi ya 900 walifikia makubaliano ya kupunguza joto duniani, baada ya jitihada za msukumo wa awali wa viongozi wa dunia kutoonesha mafanikio ya kutosha.
Miongoni mwa vikwazo vilivyokwamisha makubaliano ya awali ni nafasi ya mataifa mawili makubwa yenye kuelezwa kufanya uchafuzi mkubwa wa mazingira China na Marekani kufanya jitihada ndogo katika utekelezaji wa jitihada za ustawi wa mazingira.
China imeahidi kutekeleza majukumu yake katika makubaliano yaliyowekwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi licha ya kuwa Marekani haitoshiriki katika makubaliano hayo.
Akizungumza nchini Ujerumani Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang alikaririwa na vyombo vya habari vya kimataifa akisema kuwa nchi yake, inataka kuwa nchi ya kupigiwa mfano katika harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hata hivyo hatma ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi imeingia dosari mwishoni mwa mwezi Mei mwaka 2017 baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza nia ya kujiondoa katika makubaliano ya Paris ya mwaka 2015 kuhusu kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Nchi saba tajiri (G7) zenye maendeleo makubwa ya viwanda na demokrasia zimekutana katika mkutano wa kilele huko Sicily nchini Italia na kwamba Kati ya viongozi wa G7 ni viongozi sita tu ndiyo wamekubaliana kuunga mkono mfumo wa makubaliano ya Paris
Marekani ambalo ni Taifa kubwa lenye viwanda vingi limekataa kuunga mkono Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi ya Paris,yaliyotiwa saini miaka miwili iliyopita ili kupunguza hali ya joto duniani.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa