NCHI ya Poland iliyopo katika Bara la Ulaya inatajwa kuwa ndiyo inayoongoza katika bara hilo katika uzalishaji wa zao la mahindi ambapo hekta moja inazalisha tani 11 za mahindi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya FEERUM tawi la Tanzania David Munanka akizungumza kwenye mdahalo wa wafanyabiashara kwenye tamasha la Majimaji Selebuka amesema kwa kushirikina na nchi ya Poland FEERUM TANZANIA inatarajia kujenga maghala ya kisasa ili kuyafanya mahindi ya Tanzania kuwa na soko la kimataifa.
Munanka amesema Kampuni hiyo itatoa teknolojia ya kuhifadhi kisasa bila kutumia dawa ambayo huwezesha mahindi kukaa zaidi ya miaka mitatu bila kuharibika na kuwa na ubora wa kimataifa kama ilivyo katika nchi ya Poland.
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa nchini inayoongoza kwa uzalishaji wa zao la mahindi,hata hivyo changamoto kubwa ni ukosefu wa soko na pembejeo za kilimo hali ambayo inaleta changamoto kubwa kwa wakulima na wafanyabiashara wa mkoa huo.Mbunge wa Songea mjini Dk.Damas Ndumbaro anasema hali hiyo ndiyo iliyomsukuma kuwaleta watalaam wa kilimo toka nchini Poland wakiongozwa na Kaimu balozi wa Poland nchini Tanzania Dk.Evelina Lubieniecka ambaye alifika manispaa ya Songea kwenye mdahalo wa wafanyabiashara wa Songea.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa