SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kutoa chanjo dhidi ya Homa ya Ini aina ya B kwa watoto pamoja na watu wazima hususan walio katika hatari zaidi ya maambukizi.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhammad Bakari Kambi katika kuadhimisha kilelele cha siku ya Homa ya Ini duniani inayoadhimishwa Julai 28 kila mwaka.
“Tunaendelea kupima damu kwa ajili ya kubaini maambukizi ya virusi, vikiwemo vile vinavyosababisha Hepatitis, kabla ya wagonjwa kupatiwa damu hiyo pamoja na kutoa chanjo kwa watoto na watu wazima “ amesema Prof. Kambi
Prof. Kambi ameeleza kuwa Wananchi wa Tanzania na Afrika Mashariki wapo katika hatari ya kupata maambukizi ya Homa ya Ini, hususan aina ya B na C, kutokana na kuwa njia za maambukizi ya Virusi hivi hufanana na zile za maambukizi ya VVU. Huku akiongeza kuwa kwa sasa, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inaandaa utaratibu mzuri wa namna ya kuifikia jamii iliyobaki hasa wale walio katika hatari zaidi ya maambukizi ili kuweza kupatiwa chanjo.
“Kwa Tanzania, takwimu kutokana na tafiti chache zilizopo zinaonesha uwepo wa maambukizi ya virusi vya Homa ya Ini aina ya B na C. Mfano, kati ya wachangiaji damu 200,000 kwa mwaka 2016, asilimia 6(takriban watu 12,000) walikuwa na maambukizi ya Homa ya Ini aina ya B.”
Kwa mujibu wa takwimu za ugonjwa huo Prof. Kambi alisema kuwa Shirika la Afya Duniani kupitia ripoti ya Homa ya Ini ya mwaka 2017 zinaonesha kuwa, mnamo waka 2015 kulikuwa na vifo milioni 1.34 kutokana na Homa ya Ini ambavyo vilikuwa sawa na vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu na zaidi ya vile vitokanavyo na ugonjwa wa UKIMWI ambavyo vilikuwa milioni 1.1.
Siku ya Ugonjwa wa Homa ya Ini Duniani (World Hepatitis Day), huadhimishwa kila ifikapo tarehe 28 Julai wakati kauli mbi9u ya mwaka huu ikiwa ni “Pima, Tibu Homa ya ini
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa